Kuandaa Vifaa katika Msafara wa Tabook

Abdur Rahmaan bin Khabbaab (radhiya allaahu ‘anhu) anasimulia yafuatayo:

Nilikuwepo wakati Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipokuwa akiwahimiza Maswahabah (radhiyallahu ‘anhum) kuliandaa jeshi na kuchangia katika msafara wa Tabook. Katika tukio hilo, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) alisimama na kusema, “Ewe Mtume wa Allah (Sallallahu ‘alaihi wasallam)! Ninajitolea kuchangia ngamia mia moja na matandiko yao kamili katika njia ya Mwenyezi Mungu.”

Baada ya hapo, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akawahimiza Maswahabah (radhiya allaahu ‘anhum) kwa mara nyingine tena kuliandaa jeshi kwa ajili ya msafara wa Tabook. ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) akasimama tena na kusema, “Ewe Mtume wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam )! Ninajitolea kuchangia ngamia wengine mia mbili pamoja na matandiko yao kamili katika njia ya Mwenyezi Mungu.”

Kisha Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akawahimiza Maswahabah (radhiya allaahu ‘anhum) kuchangia katika msafara huo kwa mara ya tatu. ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) akasimama tena na akasema, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (sallallahu ‘alaihi wasallam)! Ninajitolea kuchangia ngamia wengine mia tatu pamoja na matandiko yao kamili katika njia ya Mwenyezi Mungu (hivyo kwa ujumla mchango wake wote wa ngamia ulikuwa ngamia mia sita).”

Katika tukio hilo, nilimuona Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akishuka kutoka kwenye mimbar huku Akifurahishwa sana na akisema, “Uthmaan hana haja ya kufanya kitendo kingine chochote cha wema baada ya kitendo hiki (ili kupata Jannah), Uthmaan hana haja ya kufanya kitendo kingine chochote cha wema baada ya kitendo hiki.” (Sunan Tirmizi #3700)

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …