Sura Maalum Kwenye Nyakati na Matukio Mbalimbali 4

8. Soma Surah Kahf siku ya Ijuma.

Ibnu Umar (radhiyallahu anhuma) anasimulia kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kusoma Surah Kahf siku ya ijuma, nuru (mwanga) hutoka chini ya miguu yake na kupanuka hadi kufika angani. Nuru hii itan’gaa siku ya Qiyaamah, na madhambi yake yote (madogo) atakayofanya katikati ya ijuma mbili yatakuwa yamesamehewa.”[1] 

Ali (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “Mwenye kusoma Surah Kahf siku ya ijuma (na kutekeleza haki za ijuma), atalindwa na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) kwa muda wa siku nane kutokana na kila fitnah inayoweza kutokea. Kama Dajjaal akijitokeza (katika siku nane za ulinzi wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala), basi atalindwa.”[2] 

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa’id Khudri (radhiyallahu ‘anhu): “Mwenye kusoma Surah Kahf siku ya ijuma, kama ikatokea akakutana na Dajjaal, basi Dajjaal hatoweza kumshinda au kumdhuru.”[3] 

9. Soma aya tatu za mwisho za Surah Baqarah kabla ya kulala.

Imepokewa kwamba Ali (radhiyallahu ‘anhu) alisema, “Sidhani kama mtu yoyote mwenye akili timamu atalala bila ya kusoma aya za mwisho (tatu) za Surah Baqarah, kwa sababu hakika hizo ni hazina kutoka chini ya Arsh.”[4] 


[1] رواه أبو بكر بن مردويه في تفسيره بإسناد لا بأس به كذا في الترغيب والترهيب، الرقم: 1098

[2]  المختارة للضياء المقدسي، الرقم: 429

[3] شعب الإيمان، الرقم : 2776، وقال الحاكم في المستدرك، الرقم: 8562 هذا حديث صحيح الإسناد ولم يخرجاه وقال الذهبي: صحيح

[4] سنن الدارمي، الرقم: 3427، وأخرج الإمام ابن أبي داود بإسناد صحيح على شرط البخاري ومسلم عن علي – كرم الله وجهه – موقوفا: ما كنت أرى أحدا يعقل ينام قبل أن يقرأ الآيات الثلاث الأواخر من البقرة كذا في مرقاة المفاتيح 4/1668

About admin

Check Also

Dua Baada Ya Kula 1

Dua ya kwanza: Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala) ambaye alitupa chakula na vinywaji na kutufanya Waislamu.

Dua ya pili Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala) ambaye alinipa chakula hiki kula, na alinipa bila juhudi yoyote au jitihada kutoka upande wangu.

Maelezo: Mu'aadh bin Anas (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, "Yoyote anayekula chakula chochote na baada ya hapo anasoma Dua iliyotajwa hapo juu, dhambi zake zilizopita na za baadaye (ndogo) zitasamehewa. "