Wasiwasi Wa Kuulizwa Akhera

Wakati mmoja, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) aliingia kwenye nyumba ya mnyama na akamkuta mtumwa wake akimlisha chakula ngamia. Katika kukagua malisho, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) hakufurahishwa na jinsi mtumwa wake alivyoitayarisha chakula na hivyo akamfinya sikio lake. Baada ya muda kidogo na kuchunguza matendo yake, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) aliingiwa na wasiwasi na khofu kwamba ataulizwa na kuchukuliwa hesabu kwa hatua hii huko Akhera.

Hivyo basi, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) alimwambia mtumwa huyo akisema, “Nirudishie kisasi”, lakini mtumwa akakataa kufanya hivyo. ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) aliendelea kusistiza, mpaka mtumwa alikubali na kuanza kufinya sikio lake. ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) kisha akamwambia, “Finya zaidi! mpaka akaridhika kwamba mtumwa huyo amemfikishia maumivu yale yale aliyompa mtumwa.

‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) akasema, “Ni ajabu na furaha gani iliyoje kwa adhabu inayochukuliwa katika dunia hii kabla ya kudaiwa katika ulimwengu ujao! (Al-Ahwaal libni Abid Dunya #264, Akhbaar-ul-Madiynah #1777)

Maelezo: Kumuadhibu mtumwa ilikuwa inaruhusiwa kwa ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu). Kwa hivyo, yeye alimwomba mtumwa huyo alipize kisasi kutoka kwake kwa sababu alihofia kwamba angeweza kuvuka mpaka katika kumwadhibu mtumwa huyo. Tabia hii ya ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) ilikuwa kwa hakika fikra ya khofu ya Allah Ta’ala ndani yake, na wasiwasi wa kuulizwa na kuchukuwa hesabu huko Akhera.

Allah Ta’ala atujaalie taufeeq ya kuwa na wasiwasi juu ya matengenezo yetu ya kiroho na kuchukuwa hesabu Akhera.

About admin

Check Also

Nafasi Ya Juu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Mbele Ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Baada ya kufariki kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Ma answaar walikuwa wamekusanyika huko Thaqifah Bani …