Sura Maalum Kwenye Nyakati na Matukio Mbalimbali 3

6. Soma Surah Sajdah kabla ya kulala.

Jaabir (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa halali mpaka asome Surah Sajdah na Surah Mulk.[1]

Khaalid bin Ma’daan (rahimahullah), ambae ni Taabi‘i, ametaja yafuatayo:“Hakika Sura Sajdah itabishana kaburini kwa kumtetea mwenye kuisoma. Itasema, ‘Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)! Ikiwa nipo ndani ya kitaab Chako basi ukubali uombezi wangu kwake, na ikiwa mimi si katika kitaab chako basi unifute humo!’ Sura hii itachukua maumbile ya ndege na itatandaza mabawa zake juu ya huyo mtu (ili kumlinda). Itamwombea kwa niaba yake na kumlinda kutokana na adhabu ya kaburini, na Surah Mulk pia inashiriki wema huo huo.” Imepokewa kwamba kwa ajili ya fadhila hii yenye thamani kubwa, Khaalid bin Ma’daan (rahimahullah) alikuwa akihakikisha kwamba hatolala mpaka awe amesoma Surah Sajdah na Surah Mulk.[2]

7. Soma Surah Dukhan usiku wa Alhamisi (usiku kabla ya Ijumaa).

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kusoma Surah Haa meem Ad-Dukhan katika usiku wa Ijumah (yaani usiku wa Alhamisi), madhambi yake yote (madogo) yatasamehewa.”[3]

Imepokewa kutoka kwa Abu Umaamah (radhiyallahu) kwamba Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kusoma Surah Dukhaan usiku wa kuamkia Ijumaa au Ijumaa, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) atamjengea kasri katika Jannah.”[4]


[1] سنن الترمذي، الرقم: 2892، وقال الحاكم في المستدرك 2/446: هذا حديث صحيح على شرط مسلم ولم يخرجه لأن مداره على حديث ليث بن أبي سليم عن أبي الزبير وأقره الذهبي

[2] سنن الدارمي، الرقم: 3453، وإسناده ضعيف

[3] سنن الترمذي، الرقم: 2889، وقال: هذا حديث غريب لا نعرفه إلا من هذا الوجه وعمر بن أبي خثعم يضعف قال محمد وهو منكر الحديث

[4] المعجم الكبير للطبراني، الرقم: 8026، وقال العلامة الهيثمي رحمه الله في مجمع الزوائد، الرقم: 3017: رواه الطبراني في الكبير وفيه فضال بن جبير وهو ضعيف جدا

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …