Matamanio ya Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kuhusu Wanawake Kuswali ndani ya Nyumba zao

Ingawa ilikuwa ni matamanio ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwamba watu wa Ummah wake waswali na jamaah msikitini, ilikuwa ni matamanio yake pia kwamba wanawake wa Ummah wake watimize Swalaah zao ndani ya mipaka ya nyumba zao.

Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliwahimiza wanawake kuswali ndani ya nyumba zao na kujificha machoni mwa wanaume, kiasi kwamba alisema: “Swala ya mwanamke ndani ya chumba chake ina thawabu zaidi kuliko Swalah yake katika ua ulio zuiliwa kwake, na Swalah yake ndani kabisa katika chumba chake (chumba kidogo kingine ndani ya chumba cha kulala) ina thawabu zaidi kuliko swalah yake ndani ya chumba chake.”[1]

Siku moja, Sayyidatina Ummu Humaid (radhiyallahu ‘anha), mke wa Sayyidina Abu Humaid As-Saa’idi (radhiyallahu ‘anhu), alikuja kwa Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na akasema: “Ewe Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) ninatamani kuswali nyuma yako.” Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)akajibu, “Ninatambua kwamba unatamani kuswali nyuma yangu. Lakini, Swalaah yako chumbani kwako ina thawabu zaidi kuliko Swalaah yako katika sehemu nyingine yoyote ya nyumba yako. Swalaah nyumbani kwako ina thawabu zaidi kuliko Swalaah ndani ya ua wako uliofungiwa. Swalah ndani ya ua wako uliofungiwa ina thawabu zaidi kuliko swalah yako msikitini. Swalah yako katika msikiti wa mtaa wenu ina thawabu zaidi kuliko Swalaah yako ndani ya Msikiti wangu (Musjid un Nabawi).” Sayyidatina Ummu Humaid (radhiyallahu ‘anha) ( kufuata na kutii matamanio ya Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), aliagiza kwamba pawekwe sehemu ndogo kwa ajili ya Swalah yake katika sehemu ya ndani kabisa ya chumba chake cha kulala, na atatekeleza kwa bidii Swalah zake zote hapo hadi mwisho wa maisha yake.[2]


[1] عن عبد الله عن النبي صلى الله عليه وسلم قال صلاة المرأة في بيتها أفضل من صلاتها في حجرتها وصلاتها في مخدعها أفضل من صلاتها في بيتها (سنن أبي داود، الرقم: 570)

[2] عن عبد الله بن سويد الأنصاري عن عمته أم حميد امرأة أبي حميد الساعدي أنها جاءت النبي صلى الله عليه وسلم فقالت يا رسول الله إني أحب الصلاة معك قال قد علمت أنك تحبين الصلاة معي وصلاتك في بيتك خير من صلاتك في حجرتك وصلاتك في حجرتك خير من صلاتك في دارك وصلاتك في دارك خير من صلاتك في مسجد قومك وصلاتك في مسجد قومك خير من صلاتك في مسجدي قال فأمرت فبني لها مسجد في أقصى شيء من بيتها وأظلمه وكانت تصلي فيه حتى لقيت الله جل وعلا (صحيح ابن حبان، الرقم: 2217)

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …