Kupata Dua ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) katika siku ya Ijumaa

عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: أكثروا الصلاة علي في الليلة الزهراء واليوم الأغر فإن صلاتكم تعرض علي فأدعو لكم وأستغفر (القربة لابن بشكوال، الرقم: 107، وسنده ضعيف كما في القول البديع صـ 335)

Umar Bin Khattaab (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kasema, “Zidisheni kunitumia salaa na salaam juu yangu katika usiku na mchana wa Ijumaah. Hakika salaa na salaam zenu zinaletwa kwangu. Kisha mimi nawaombeeni dua na kumuomba Allah subhaana wata’ala awasamehe madhambi yenu.

Utukufu Na Heshima Kwa Nywele Zilizobarikiwa Za Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Abu Hafs, Umar bin Hasan Samarqandi (rahimahullah), anasimulia tukio lifuatalo katika kitaab chake, Rownaqul Majaalis:

Wakati fulani kulikuwa na mfanyabiashara tajiri ambaye aliishi katika jiji la Balkh na alikuwa na watoto wawili. Baada ya kifo chake, wanawe wawili waligawanya mali kati yao kwa usawa.

Iliyojumuishwa katika mali hiyo kulikuwa na nywele tatu zilizobarikiwa za Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Katika kuganywa kwa mali, kila mtoto alichukua nywele mmoja, na kuacha nywele ya tatu ukiwa wa wote wawili. Basi, kaka mkubwa akapendekeza na kusema, “Na tukate hii nywele ya tatu kuwa nusu ili kila mmoja achukue sehemu yake kutoka kwenye nywele huo.” Lakini, kaka mdogo hakukubaliana na msemo huu, “Hapana! Wallahi, heshima tunayotakiwa kumuonyesha Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) ni kwamba haifai sisi kukata nywele zake zilizobarikiwa. Wakati kaka mkubwa aliposhuhudia upendo na heshima aliyokuwa nayo mdogo wake kwa nywele zilizobarikiwa za Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alipendekeza, “Kwa nini usichukue nywele zote tatu alafu niachie mimi urithi?” Kwa kumpenda Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kaka mdogo alikubali. Ikatokea hivyo, kaka mkubwa alichukua mali yote ya urithi huku kaka mdogo akichukua tu nywele tatu za nywele.

Kaka mdogo aliziweka mfukoni kwa heshima kubwa. Baada ya hapo, mara kwa mara alikuwa akizitoa mfukoni mwake, na kuzitazama kwa upendo na kumtumia salaam Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Kisha akizirudisha mfukoni mwake.

Baada ya muda kupita, mali yote ya kaka mkubwa ilikuwa imepungua, ambapo kaka mdogo alipewa mali nyingi na Allah Ta’ala. Lakini, baada ya muda, kaka mdogo alikufa.

Baada ya kuondoka katika dunia hii, mtu mchamungu mmoja aliota ndoto ambayo alimuona mdogo wake pamoja na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam).

Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akamwambia yule mchamungu na kusema, “Wambie watu kwamba ikiwa yoyote ana haja kutoka kwa Allah Ta’ala, aende kwenye kaburi la mtu huyu (akimaanisha mdogo wake) na aombe dua kwa Allah Ta’ala kumtimizia haja zake. Mahitaji yake yote yatakuwa yametimiziwa.”

Watu walikuwa wakija kwenye kaburi la ndugu huyu ili kuomba dua, mpaka hata wale waliokuwa wakipita na usafiri zao walikua wakishuka na kutembea kwa miguu kwa heshima kabla ya kufika kaburini.

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …