Kupata Maombezi Ya Nabii Wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

عن أبي الدرداء قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من صلى علي حين يصبح عشرا وحين يمسي عشرا أدركته شفاعتي يوم القيامة (رواه الطبراني بإسنادين وإسناد أحدهما جيد ورجاله وثقوا كذا في مجمع الزوائد، الرقم: ١٧٠٢٢)

Sayyidina Abu Dardaa (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “yoyote ambaye atakaye nitumie salaam mara kumi asubuhi na mara kumi jioni, atapata msaada wangu siku ya qiyama.”

Tiba Ya Allaamah Qastallani (rahimahullah)

Allaamah Qastallani (rahimahullah), mwanachuoni mashuhuri wa Hadith, anaandika katika kitaab chake ‘Mawaahib Ladunni’:

Wakati fulani, niliugua sana mpaka madaktari walikata tamaa juu ya afya yangu, na nilibaki katika hali hii kwa miaka mingi. Basi siku moja, tarehe 28 Jumaadul Ulaa 893 B.H (Baada ya Hijra) nikiwa Makka Mukarramah, nilimuomba Allah Ta’ala kupitia Wasila wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), kwamba Allah Ta’ala Aniponye na ugonjwa wangu.

Nilipokuwa usingizini, niliona maono ambayo nilimwona mtu akiwa na kipande cha karatasi mkononi ambacho kiliandikwa juu yake. “Nabi Wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) ameamrisha kwamba dawa hii apewe Ahmad bin Qastallani.” Nilipoamka nilikuta hakuna dalili ya ugonjwa wowote Uliobaki.”

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …