Kabla Ya Swalaah

5. Kabla ya kuanza kuswali, hakikisha kwamba mavazi yako ni ya heshima na sio yakubana. Epuka kuvaa mavazi ambayo hayana heshima badala vaa mavazi ambayo yanazingatia na utakatifu wa Swalaah, na pia epuka na mavazi ambayo yana picha au maandishi juu yake.[1]

6. Hakikisha kwamba unaswali kwa kuvaa kofia (ya kiislamu) kwa sababu ilikuwa ni desturi na Sunnah ya Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na Maswahaaba (radhiyallahu ‘anhum) kuswali huku akiwa wamevaa kofia.

روي عن ابن عباس رضي الله عنهما أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يلبس القلانس تحت العمائم ويلبس العمائم بغير القلانس (جمع الوسائل صـ 207)[2]

Sayyidina Abdullah bin Abbaas (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa akivaa kofia chini ya kilemba, na kuna wakati alikuwa akivaa kilemba tuu bila ya kofia.

قال الحسن كان القوم يسجدون على العمامة والقلنسوة (صحيح البخاري 1/56)[3]

Sayyidina Hasan Basri  (rahimahullah) anasema, “Maswahaabah (radhiyallahu ‘anhum) walikuwa wakisujudu wakati wa Swalaah juu ya vilemba na kofia zao.”


[1] ويسن للرجل أن يلبس للصلاة أحسن ثيابه (الإقناع في حل ألفاظ أبي شجاع 1/124)

وتكره الصلاة في الثوب الذي عليه الصورة (المجموع شرح المهذب 3/129)

[2] لهذا الحديث شواهد

[3] عن الحسن أن أصحاب رسول الله صلى الله عليه وسلم كانوا يسجدون وأيديهم في ثيابهم ويسجد الرجل منهم على قلنسوته وعمامته وهكذا رواه عبد الرزاق موصولا عن هشام بن حسان عن الحسن ورواه أيضا ابن أبي شيبة من طريق هشام (فتح الباري 1/588)

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …