Kupata Ukaribu Maalumu Wa Nabii Wa Allah (sallallahu ‘alaihi wassallam) Siku Ya Kiama

عن عبد الله بن مسعود أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: أولى الناس بي يوم القيامة أكثرهم علي صلاة (سنن الترمذي، الرقم: ٤٨٤، وحسنه الإمام الترمذي رحمه الله)

Sayyidina Abdullah Bin Mas’ood (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kuwa Nabii wa Allah(sallallahu ‘alaihi wassallam) amesema “mtu ambaye atake kuwa karibu sana na mimi (ambae anastahili sana msamaha wangu) siku ya kiama ni yule ambae alikuwa ananiswalia sana duniani.”

Upendo wa dhati wa Umar (radhiyallahu ‘anhu) na Kumbukumbu kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Usiku mmoja, Umar (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa kwenye uchunguzi wake wa usalama wakati aliona mwanga na kusikia sauti ikitoka kwenye nyumba fulani. Alimkuta bibi kizee ndani yake akisokota sufu na kuimba mashairi ambayo maana yake ni ifuatavyo:

“Allah ta’ala azikubali dua za wachamungu, kumtakia baraka Muhammad (sallallahu alaihi wasallam).

“Ewe Mjumbe wa Allah Ta’ala, ulikuwa ukiabudu kila usiku, na ulikuwa ukilia kabla ya alfajiri ya kila siku.

“Natamani kujua kama ningeweza kuwa pamoja na mpendwa wangu (Sallallaahu ‘alaihi wasallam), kwani kifo kinakuja katika hali tofauti na sijui nitakufa vipi.”

Aliposikia mashairi haya, Umar (radhiyallahu ‘anhu) aliketi chini, akilia tika kumpenda na kumkumbuka Nabii Wa Allah (sallallahu alaihi wasallam).(Kitaab Zuhdi libnul Mubaarak, #1023)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …