Ushujaa wa Ali (Radhiyallahu ‘anhu) katika Uhud

Wakati wa vita vya Uhud, Maswahabah (radhiya Allaahu ‘anhum) walishambuliwa na makafiri na wengi kuuawa. Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) alizungukwa na maadui na alipata majeraha kadhaa. Wakati huo, uvumi ulianza kuenea kwamba Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) ameuawa. Kusikia uvumi huu wa uongo, wengi wa Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) walipoteza utulivu na waliingiwa na huzuni mkubwa na wasiwasi.

Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasema: “Tulikuwa tumezungukwa na maadui, na sikuweza kumuona Rasulullah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Nilimtafuta kwanza kati ya walio hai na kisha kati ya waliofariki, lakini sikuweza kumpata. Nilijiambia, ‘Haiwezekani kwake kukimbia kutoka uwanja wa vita. Inaonekana kuwa Allah Ta’ala ametukasirikia kwa sababu ya madhambi zetu, na amemnyanyua mbinguni. Hakuna kitu bora kwangu kuliko kujirusha kwenye safu za adui na kupigana mpaka niuawe.’

“Basi nikawashambulia maadui, hata wakaanza kutawanyika. Baada ya hapo macho yangu yakamfikia Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) katika uwanja wa vita. Nilipomuona, niliingiwa na furaha na nikaelewa kwamba Allah Ta’ala amekuwa akimlinda kupitia malaika wake. Nilimsogelea na kusimama pembeni yake. Hapo hapo, kundi la maadui lilisonga mbele kumshambulia Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam). Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akaniambia, ‘Ewe Ali, nenda ukawafukuze! yao. .baada ya hayo, kundi jingine likaja kumshambulia. Akaita tena, ‘Ewe Ali, nenda ukawaondowe!’ Nikapigana na kundi hilo tena, kwa mkono mmoja, mpaka nikawaondoa, na kuwafanya kukimbia.

Ni katika tukio hili ambapo Jibrail (‘Alayhis salaam) alikuja kwa Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na akamsifu Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwa ushujaa na kujitolea kwake kwa Rasulullah (Sallallahu’alaihi wasallam). Mtume (Sallallahu’alaihi wasallam) amesema:

إنه مني وأنا منه

“Ali katoka kwangu na mimi nimetoka kwake (yaani sisi tunatoka katika familia moja na uhusiano wetu wa udugu uko karibu sana).”

Kwa hili, Jibrail (‘Alayhis Salaam) alisema:

وأنا منكما

“Na Mimi ni miongoni yenu nyote wawili.”

Tazama ushujaa wa Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu)! Wakati Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alimuelekeza kuwafukuza maadui, alijitupa kwenye safu za maadui na akapigana mkono mmoja kwa ushujaa kama huo ili kuwazuia maadui wasimdhuru Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam). Hii inaonyesha mapenzi yake yaliyopitiliza na kujitolea kwake kwa Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam).

About admin

Check Also

Nafasi Ya Juu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Mbele Ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Baada ya kufariki kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Ma answaar walikuwa wamekusanyika huko Thaqifah Bani …