Monthly Archives: December 2022

Msaada Katika Daraja La Swirat

Sayyidina Abur Rahmaan Bin Samurah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti: wakati mmoja, Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuja kwetu na akasema, "usiku wa jana, niliona kitu cha maajabu kwenye ndoto nilimuona mtu katika umati wangu alikuwa anavuka daraja la swiraat (daraja juu ya jahannam). Kuna wakati alikuwa anatambaa, wakati mwingine, alikuwa anajiburuza kwa makalio yake, wakati mwingine, alikuwa ananing'inia kwenye daraja la swiraat (karibu ya kuanguka ndani ya jahannam). Ghafla, salam zake alizokuwa ananisalia mimi duniani zimemfikia. Zikaja zikamshika mkononi, zilimsaidia kusimama katika daraja la swiraat na zikamsaidia kuvuka juu yake."

Soma Zaidi »