Msaada Katika Daraja La Swirat

عن عبد الرحمن بن سمرة قال: خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم فقال: إني رأيت البارحة عجبا رأيت رجلا من أمتي قد احتوشته ملائكة فجاءه وضوؤه فاستنقذه من ذلك ورأيت رجلا من أمتي قد احتوشته الشياطين فجاءه ذكر الله فخلصه منهم ورأيت رجلا من أمتي يلهث عطشا من العطش فجاءه صيام رمضان فسقاه ورأيت رجلا من أمتي بين يديه ظلمة ومن خلفه ظلمة وعن يمينه ظلمة وعن شماله ظلمة ومن فوقه ظلمة ومن تحته ظلمة فجاءه حجه وعمرته فاستخرجاه من الظلمة ورأيت رجلا من أمتي جاءه ملك الموت يقبض روحه فجاءه بره بوالديه فرد عنه ورأيت رجلا من أمتي يكلم المؤمنين ولا يكلموه فجاءته صلة الرحم فقالت إن هذا واصل كان واصلا لرحمه فكلمهم وكلموه وصار معهم ورأيت رجلا من أمتي يأتي الناس وهم حلق فكلما أتى على حلقة طرد فجاءه اغتساله من الجنابة فأخذه بيده فأجلسه معهم ورأيت رجلا من أمتي يتقي وهج النار بيديه عن وجهه فجاءته صدقته وصارت ظلا على رأسه وسترا على وجهه ورأيت رجلا من أمتي جاءته زبانية العذاب فجاءه أمره بالمعروف ونهيه عن المنكر فاستنقذه من ذلك ورأيت رجلا من أمتي هوى في النار فجاءته دموعه التي بكى من خشية الله فأخرجته من النار ورأيت رجلا من أمتي قد هوت صحيفته إلى شماله فجاءه خوفه من الله فأخذ صحيفته فجعلها في يمينه ورأيت رجلا من أمتي يرعد كما ترعد السعفة فجاءه حسن ظنه بالله فسكن رعدته ورأيت رجلا من أمتي يزحف على الصراط مرة ويجثو مرة ويتعلق مرة فجاءته صلاته علي فأخذت بيده فأقامته على الصراط حتى جاوز ورأيت رجلا من أمتي انتهى إلى أبواب الجنة فغلقت الأبواب دونه فجاءته شهادة أن لا إله إلا الله فأخذته بيده فأدخلته الجنة (الأحاديث الطوال للطبراني صـ ٢٧٣، وإسناده ضعيف كما في مجمع الزوائد، الرقم: ١١٧٦٤)

Sayyidina Abur Rahmaan Bin Samurah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti: wakati mmoja, Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuja kwetu na akasema, “usiku wa jana, niliona kitu cha maajabu kwenye ndoto nilimuona mtu katika umati wangu alikuwa anavuka daraja la swiraat (daraja juu ya jahannam). Kuna wakati alikuwa anatambaa, wakati mwingine, alikuwa anajiburuza kwa makalio yake, wakati mwingine, alikuwa ananing’inia kwenye daraja la swiraat (karibu ya kuanguka ndani ya jahannam). Ghafla, salam zake alizokuwa ananisalia mimi duniani zimemfikia. Zikaja zikamshika mkononi, zilimsaidia kusimama katika daraja la swiraat na zikamsaidia kuvuka juu yake.

Kusafiri kwa ajili ya Hadith Moja

Kathir bin Qais (rahimahullah) anaripoti:

Siku moja nilikuwa nimekaa na Abu Dardaa (radhiyallahu ‘anhu) katika msikiti mmoja huko Damascus, mtu mmoja alipomjia na kusema: “Ewe Abu Dardaa, nimesafiri kutoka Madinah Tayyibah kuja kupata Hadith moja kutoka kwako, kama nilivyosikia kwamba wewe umeisikia hadithi moja kwa moja kutoka kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam).

Abu Dardaa… akauliza, “Je, hauna kazi nyingine yoyote huku Damascus?” Yule mtu akajibu, “Hapana (yaani nimekuja Damascus tu kuchukua Hadith).” Abu Dardaa (radhiyallahu ‘anhu) akauliza tena, “Je, una uhakika kwamba huna kazi nyingine huko Damascus?” Mtu huyo akajibu tena, “Nimekuja mahali hapa na lengo tu la kujifunza Hadith hii.”

Abu Dardaa (radhiyallahu ‘anhu) kisha akasema, “Sikiliza, nimemsikia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akisema: ‘Allah Ta’ala humrahisishia njia ya kwenda Peponi kwa yule anae safiri mbali kiasi kutafuta elimu. Malaika wanakunjua mbawa zao chini ya miguu yake, na kila kilichomo mbinguni na ardhini (hata samaki ndani ya maji) kinamuombea msamaha kwa Allah Ta’ala. Ubora na daraja ya juu ya mtu mwenye elimu ya Dini juu ya mtu anayeshughulika na ibada (bila ya kuwa na elimu ya Deeni) ni kama ubora wa mwezi juu ya nyota. Ulamaa (masheikhe) ndio warithi wa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Urithi wa manabii si dhahabu wala fedha. Badala yake, urithi wao ni elimu ya Dini. Mwenye kupata elimu ya Dini hakika amepata mali nyingi.”

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …