Sahaabah

Dua ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa Ali (radhiya allaahu ‘anhu) wakati wa Kumtuma kwenda Yemen

Ali (radhiya allaahu ‘anhu) anaripoti: Rasulullah (sallallahu ‘alahi wasallam) alinituma kama waziri wake kwenda Yemen. Kabla ya kuondoka, nilimwambia, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (sallallahu ‘alaihi wasallam)! Unanipeleka kwa watu ambao ni wakubwa kuliko mimi. Zaidi ya hayo, mimi ni kijana na sina ufahamu wowote katika uwanja wa Qadhaa (mambo …

Soma Zaidi »

Kununua Ardhi kwa ajili ya Upanuzi wa Masjid-ul-Haram

Wakati mmoja, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alimwendea mtu fulani huko Makka Mukarramah na kumwambia, “Ewe fulani! Je, utaniuzia nyumba yako, ili nipanue eneo la msikiti karibu na Al-Ka’ba, na kwa malipo ya tendo hili jema, nitakudhaminia kasri katika Jannah (yaani zaidi ya pesa utakazopokea ya nyumba hii)?” Yule mtu akajibu, …

Soma Zaidi »

Kuandaa Vifaa katika Msafara wa Tabook

Abdur Rahmaan bin Khabbaab (radhiya allaahu ‘anhu) anasimulia yafuatayo: Nilikuwepo wakati Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipokuwa akiwahimiza Maswahabah (radhiyallahu ‘anhum) kuliandaa jeshi na kuchangia katika msafara wa Tabook. Katika tukio hilo, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) alisimama na kusema, “Ewe Mtume wa Allah (Sallallahu ‘alaihi wasallam)! Ninajitolea kuchangia ngamia mia moja …

Soma Zaidi »

Wasiwasi Wa Kuulizwa Akhera

Wakati mmoja, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) aliingia kwenye nyumba ya mnyama na akamkuta mtumwa wake akimlisha chakula ngamia. Katika kukagua malisho, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) hakufurahishwa na jinsi mtumwa wake alivyoitayarisha chakula na hivyo akamfinya sikio lake. Baada ya muda kidogo na kuchunguza matendo yake, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) aliingiwa …

Soma Zaidi »

Fadhila Kumi Maalum Za ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu)

Abu Thowr (rahimahullah) anasimulia kwamba siku moja alikuja kwa ‘Uthmaan (radhiya allahu ‘anhu) na kumsikia akitaja yafuatayo wakati ukosoaji usio sahihi ulipokuwa ukitolewa dhidi yake. Alisema: Kuna mema kumi ambayo nimeyalinda kwa Allah Taala na kwa kila amali natarajia kupata malipo ya Akhera; 1) Nilikuwa mtu wa nne kusilimu. 2) …

Soma Zaidi »

Hofu Ya Uthman (radhiyallahu ‘anhu) kwa ajili ya Akhera

Haani (rahimahullah), mtumwa aliyeachwa huru wa ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu), anataja kwamba wakati ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) anaposimama kaburini, alikuwa akilia sana hadi ndevu zake zikilowa kwa machozi yake. Mtu mmoja akamuuliza, “Tunaona kwamba unapokumbuka Jannah na Jahannam na kuzijadili, hauathiriki hadi unaanza kulia, lakini unaposimama kaburini tunakuona unaingiwa na …

Soma Zaidi »

Kuwa Mlaini na Mpole Unapojishughulisha na Watu:

‘Ataa bin Farrookh (rahimahullah) anasimulia yafuatayo: Wakati mmoja, ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) alinunua kiwanja kutoka kwa mtu fulani. Baada ya kununua ardhi, ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimsubiri mtu huyo aje kuchukua pesa zake. Lakini mtu huyo hakuja. ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu) alipokutana na mtu huyo baadaye, alimuuliza, “Kwa nini hukuja …

Soma Zaidi »

Hayaa ya ‘Uthmaan (radhiya allaahu ‘anhu)

‘Aaishah (radhiya allaahu ‘anha) anasimulia yafuatayo: Wakati mmoja, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa amelala chini nyumbani kwangu na kanzu yake ilihamishwa kidogo kutoka eneo la paja lake au goti lake, ingawa paja lake na goti yalifunikwa na kikoyi chake. Wakati huo, Abu Bakr (radhiya allaahu ‘anhu) aliomba ruhusa ya kuingia. …

Soma Zaidi »

Bashara Za Jannah

Abu Muusa (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasimulia yafuatayo: Wakati fulani nilikuwa na Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) katika bustani mmoja wa Madina Munawwarah alipokuja mtu na kuomba ruhusa ya kuingia kwenye bustani hiyo. Aliposikia ombi la mtu huyo, Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akaniambia: “Mruhusu aingie na umpe bashara ya daraja la juu …

Soma Zaidi »

Muislamu Wa Kwanza Kufanya Hijrah Pamoja Na Familia Yake

Anas (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa ameondoka kwenda Abyssinia, akihijiria pamoja na mke wake mheshimiwa, Ruqayyah (radhiyallahu ‘anha), binti Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam). Habari za hali yao zilicheleweshwa, na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akawa na wasiwasi na alikuwa akitaka kutoka Makkah Mukarramah kupata habari zao. Hatimaye, mwanamke …

Soma Zaidi »