Wakati mji wa Damascus ulipofikia mikononi mwa Waislamu, Abu Ubaidah (Radhiyallahu ‘Anhu) – Kamanda wa Jeshi la Waislamu – alimchagua Sa’eed bin Zaid (Radhiyallahu’ Anhu) kama waziri juu ya Jiji la Damascus.
Baada ya hapo, Abu Ubaidah (Radhiyallahu ‘Anhu) aliendelea na jeshi lake kuelekea Jordan. Baada ya kufikia Jordan, walipanga kambi hapo na kuanza kufanya maandalizi ya kukabiliana na madui. Abu Ubaidah (Radhiyallahu Anhu) alimchagua Khalid bin Waleed na Yazid bin Abu Sufyaan (radhiyallahu anhuma) kama ma comanda juu la jeshi.
Wakati Sa’eed bin Zaid (Radhiyallahu ‘Anhu) alipofahamishwa kuwa Jeshi la Waislamu litakuwa vitani na makafiri, hamu kubwa iliingia moyoni mwake ili kujiunga na Jeshi la Waislamu na ajitolee Maisha yake kwa ajili ya Allah Ta’ala.
Akishikwa na hamu hii kubwa, aliandika barua kwa Abu Ubaidah (Radhiyallahu ‘Anhu) ambayo alionyesha hamu yake ya kujiunga katika Jihaad na pia aliomba aondolewe kama waziri juu ya Dameski.
Baada ya kumsifu Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) na kumtumia Salaam, aliandika yafuatayo katika barua hiyo kwa Abu Ubaidah (Radhiyallahu Anhu): “Kwa kuzingatia kushiriki katika Jihaad, siwezi kubaki nyuma na kukupa wenzako upendeleo juu yangu, haswa wakati Jihaad ni njia ya mimi kupata Radhi (na ukaribu wa) wa mola wangu. Kwa hivyo, mara tu unapopokea barua yangu hii, tafadhali mchague mtu mwengine kwenye nafasi yangu ambaye ana hamu kubwa ya kusimamia jukumu hili kuliko mimi, kwani hivi karibuni nitajiunga na Jeshi, Inshallah. ”
Wakati barua ya Sa’eed bin Zaid (Radhiyallahu ‘Anhu) ilimfikia Abu Ubaidah (Radhiyallahu’ Anhu), alisema: “Yeye (Sa’eed) amedhamiria kuacha nafasi yake (na ajiunge na jeshi la Jihaad, kwa hivyo hatuwezi kumzuia sasa).” Kisha akamwita Yazeed bin Abu Sufyaan (Radhiyallahu ‘Anhu, kamanda wake mkuu) na akamwagiza amchague mtu kama waziri wa damascus, badala ya Sa’eed (Radhiyallahu ‘Anhu). (Ar riyaadhun nadhrah fi manaaqibil ‘ashrah 4/343)