Malaika wanasafiri duniani kukusanya salaam.

عن عبد الله قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: إن لله ملائكة سياحين في الأرض يبلغوني من أمتي السلام (سنن النسائي، الرقم: 1282، صحيح ابن حبان، الرقم: 913)

Abdullah Bin Ma’sood (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Kasema, “hakika, Allah subhaana wata’ala ana kundi la malaika wanaotangatanga (kote ulimwenguni ili waweze kutafuta mikusanyiko ya watu wakimswalia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)) na kufikisha salaam za umma wangu kwangu.”

Qaseedah Burdah

Allaamah Busairi (rahimahullah ) Alikuwa msomi wa Deen na mchamungu. Ndani ya maisha yake, alipatwa na strok. Aliandaa mashairi yake ( Qaseedah Burdah) kwa matumaini kwamba mashairi haya ya sifa na upendo wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) yatakuwa njia ya yeye kutafuta rehema za Allah na kumponesha kutoka kwenye ugonjwa wake.

Usiku mmoja, alimwona Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) katika ndoto na akapeleka mbele ya Rasulullah mashairi aliyoyatunga kwa upendo wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Aliweka mkono wake wa baraka juu yake, na alipoamka asubuhi, alikuwa amepona na kuweza kutembea. (kasfuz zonoon 2/1331)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …