Fitnah za kuenea za Dajjaal vipo katika vitabu vya Aqaa’id (imani za Kiisilamu). Ulama wa aqida wanamakubaliano kwamba kuamini katika kutokea kwa Dajjaal ni katika Aqida ya Ahlus Sunnah Wal Jamaa’ah.
Ahaadith ambazo Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alikuwa ameonya Ummah kuhusu Fitnah za Dajjaal ni nyingi sana kwamba vitabu vya aqida zote zimeeleza kwamba kuamini katika kuja kwa Dajjaal kuwa miongoni mwa imani za Ahlus Sunnah Jamaah. Kwa hivyo, wanazuoni wakubwa wamewachukulia wale ambao wamekataa kuja kwa Dajjaal kuwa miongoni mwa madhehebu yaliyopotoka kama vile Wa Khawaarij, Wa Mu’tazilah, nk.
Allaamah Suyooti (Rahimahullah) anaeleza, ikiwa mtu atakataa hadithi ambazo zinathibitisha uwepo wa Dajjaal, mtu atakuwa Kafiri. Hii inapatikana kutoka katika Hadith ifuatayo ya Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam):
من كذب بالدجال فقد كفر ومن كذب بالمهدي فقد كفر
Yule anayemkataa Dajjaal amekufuru, na yule anayemkataa Mahdi (Radhiyallahu ‘Anhu) amekufuru. (Al-Qowl-ul-Mukhtasar pg. 16)
Imani ya Ahlus Sunnah Wal Jamaa’ah ni kwamba Dajjaal ni mwanadamu maalum.
Muhaddith mashuhuri, Allaamah Qaadhi Iyaaz (Rahimahullah), ameelezea wazi kuwa imani ya Ahlus Sunnah Wal Jamaa ni kwamba Dajjaal ni mwanadamu maalum. Allaamah Qaadhi Iyaaz (Rahimahullah) alisema:
Hizi ahaadith ambazo Imaam Muslim (Rahimahullah) na wengine walisimuliya kuhusu Dajjaal ni dhibitisho kwa wale ambao wako kwenye njia ya Haq, kuanzisha uwepo wa Dajjaal na kwamba yeye ni mwanadamu maalum. Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) atamleta kama fitna kwa watumishi wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) na kumpa uwezo wa kutekeleza vitendo visivyo kawaida, kama vile kuwapa uhai kwa watu walio fariki ambao alikuwa amewaua, akileta vitu vizuri ulimwenguni na kusababisha ardhi tasa kuwa nyepesi, kuwa na vitu vya Faraja na adhabu na mito (ambayo atasababisha kutiririka), na kufanya utajiri wa dunia kumfuata, na kuamuru anga kunyesha na dunia kutoa mazao. Haya matendo yote visio vya kawaida zitajidhihirisha na uwezo wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) na idhini yake. Baada ya hapo, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) atasababisha nguvu zake zote za dajjal kupotea, na hataweza kumuua mtu huyo (ambaye alikuwa amemuua na kumrudisha, kama ilivyotajwa katika Hadith), wala mtu mwingine yeyote. Nabi Isa (‘Alaihis Salaam) atamuua na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) atawabariki waumini kwa uthabiti juu ya Dini. Haya ni maoni ya Ahlus Sunnah Wal Jamaa’ah, na Muhadditheen wote, Fuqahaa na Ulama wa Aqida, kinyume na wale ambao wanamkataa Dajjaal kama vile madhehebu ya Khawaarij, Jahmiyyah na baadhi ya Mu’tazilah.