Sunna Na Adabu Za Dhul Hijjah 4

7. Siku ya Arafah, mtu anapaswa kujihusisha na Dua. Siku hii ni Siku ya Barakah, iliyobarikiwa zaidi kuliko siku zingine kumi za Dhul Hijjah. Inaripotiwa kwamba Ali (Radhiyallahu anhu) alisema kuwa katika siku hii, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) huwaachisha watu huru kutoka Moto wa Jahannum zaidi kuliko siku nyingine yoyote. Ali (Radhiyallahu anhu) pia alikuwa akiomba Dua ifuatayo siku ya Arafah na kuhamasisha wenzake kuomba Dua hio hio:

اَللّٰهُمَّ أَعْتِقْ رَقَبَتِيْ مِنَ النَّارِ وَأَوْسِعْ لِيْ مِنَ الرِّزْقِ الْحَلالِ وَاصْرِفْ عَنِّيْ فَسَقَةَ الْجِنِّ وَالْإِنْسِ

Ee Mwenyezi Mungu! Aachisha shingo langu huru kutoka moto wa Jahannum, unibariki na rizki ya halali kwa wingi, na uwaondoe watu na majini wabaya kwangu.[2]

8. Haaji (mtu ambae anahiji) anapaswa kusoma mara mia moja yafuatayo wakati wa kufanya wuqoof huko Arafah tarehe 9:

لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيْكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلٰى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

Hakuna mungu apasaye kuabudiwa isipokuwa Allah Ta’ala, ambaye hana mwenzi. Kwake ni ufalme (wa ulimwengu wote), na kwake yeye ni sifa zote. Katika mikono yake (udhibiti) peke yake ni mazuri yote na yeye peke yake ana nguvu kamili juu ya kila kitu.

Baada ya hapo, anapaswa kusoma Surah Ikhlaas (Qul Huwallah) mara mia, ikifuatiwa na salaa na salaam ifuatayo mara mia moja:

اَللَٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ كَمَا صَلَّيْتَ عَلٰى إِبْرَاهِيْمَ وَآلِ إِبْرَاهِيْمَ إِنَّكَ حَمِيْدٌ مَّجِيْدٌ وَعَلَيْنَا مَعَهُمْ

Ee Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad (Sallallahu alaihi wasallam), kama ulivyomrehemu Nabi Ebrahim (alaihis salaam) na familia ya Nabi Ebrahim (alaihis salaam) hakika wewe ni mwenye kusifiwa zaidi, mwenye utukufu zaidi, na uturehemu sisi pamoja nao.

Jaabir (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema kwamba wakati Mwislamu yoyote anayesimama jioni wa siku ya Arafah sehemu ya wuqoof, akielekea qiblah, na akasoma dhikri iliyotajwa hapo juu, kish Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) anasema:

“Enyi malaika zangu! Je! Ni malipo gani kwa mtumwa wangu kwa kusoma hili? Amenitukuza, akashuhudia umoja wangu, alitaja ukubwa wangu, akaniheshimu, akanitambua, akanisifu na kutuma salamu juu ya Mtume wangu. Mshuhudie, Enyi malaika zangu, kwamba nimemsamehe na kumpa heshima ya shafaa’ah, na ikiwa angewaombea watu hawa wote ambao wamesimama hapa, ningekubali maombezi yake. “[2]


[1] ومنها كثرة الدعاء بالمغفرة والعتق فإنه يرجى إجابة الدعاء فيه روى ابن أبي الدنيا بإسناده عن علي قال ليس في الأرض يوم إلا لله فيه عتقاء من النار وليس يوم أكثر فيه عتقا للرقاب من يوم عرفة فأكثر فيه أن تقول: اللهم أعتق رقبتي من النار وأوسع لي من الرزق الحلال واصرف عني فسقة الجن والإنس فإنه عامة دعائي اليوم (لطائف المعارف صـ 284)

[2] شعب الإيمان، الرقم: 3780، وقال: هذا متن غريب وليس في إسناده من ينسب إلى الوضع والله أعلم

About admin

Check Also

Sunna na Aadaab za Jumu’ah 4

12. Jitahidi kumswalia Mtume (sallallahu alaihi wasallam) mara elfu moja siku ya Jumu’ah. Anas (Radhiyallahu …