3. Jitahidi kufanya ibaadah nyingi iwezekanavyo wakati katika siku kumi za kwanza za dhul hijjah. Kufanya Ibaadah katika hizi siku utapata thawabu sawa sawa na kufanya Ibaadah ndani ya Lailatul Qadr.
Abu Hurairah (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Hakuna siku ndani ya mwaka ambayo Ibada inapendwa zaidi na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) kuliko siku kumi za dhul hijjah. Swaumu ndani ya hizi siku (ukitoa siku ya kumi) ni sawa na kufunga mwaka mzima, na kusimama katika Ibaadah ndani ya siku hizi ni sawa na thawabu ya usiku wa Lailatul Qadr.”[1]
Hafsah (Radhiyallahu anha) anasema kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) hakuacha matendo manne ; Kufunga siku ya Aashuraa, kufunga siku kumi za kwanza za dhul Hijjah (ukitoa siku ya kumi), kufunga siku tatu za kila mwezi; na kuswali Rakaah mbili za Sunnah kabla ya alfajri.[2]
4. Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema kwamba jannah inakuwa Waajib Kwa yule ambaye anayemwabudu Allah Ta’ala ndani ya usiku tano yaani: usiku wa Tarwiyah (tarehe 8 wa dhul hijjah), usiku wa Arafah (tarehe 9 wa Dhul Hijjah), usiku wa Nahr (tarehe10 wa Dul Hijjah), usiku wa Eidul Fitr (idi ndogo) na usiku wa 15 wa Sha’baan.
Muadh bin Jabal (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Yule anauhaisha usiku tano ndani ya mwaka na Ibaadah, Jannah inakuwa wa lazima kwake. (Usiku tano hizi ni) usiku wa tarwiyah (tarehe 8 wa Dul hijjah), usiku wa arafah (tarehe 9 wa dhul hijjah), usiku wa Nahr (tarehe 10 wa dhul hijjah), usiku ya Eidul Fitr na usiku wa 15 wa Sha’baan.”[3]
[1] سنن الترمذي، الرقم: 758، وقال: هذا حديث غريب
[2] سنن النسائي، الرقم: 2416، صحيح ابن حبان، الرقم: 6422
[3] تاريخ ابن عساكر 43/93، وقد ذكره المنذري في الترغيب والترهيب، الرقم: 1656، بلفظة “عن”، إشارة إلى كونه صحيحا أو حسنا أو ما قاربهما عنده كما بين أصله في مقدمة كتابه 1/50