Rasulullah (Sallalllahu ‘Alaihi Wasallam) akimchagua Abdur Rahmaan bin Auf (Radhiyallahu’ Anhu) kama kiongozi wa Jeshi kwenda Dumatul Jandal

Katika mwaka wa sita baada ya Hijrah, wakati wa mwezi wa Sha’baan, Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alimhutubia Abdur Rahmaan bin Auf (Radhiyallahu ‘Anhu) na kumwambia, “Fanya maandalizi Kusafiri, ninakaribia kukutumia kwenye safari ima leo au kesho Insha Allah. ”

Asubuhi iliyofuata, wakati Abdur Rahmaan bin Auf (Radhiyallahu ‘Anhu) alipokuja kabla Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam), alikuwa amevaa kilemba nyeusi. Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alifungua kilemba chake na akairudisha nyuma ya kichwa chake, na mkia ukining’inia nyuma ya mgongo wake. Urefu wa mkia ulikuwa takriban urefu wa vidole vinne. Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) kisha akamwambia: “Ewe ibnu auf, hii ndio jinsi unapaswa kuvaa kilemba, kwa sababu hii ndio njia ya Waarabu na ni bora. ”

Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alimchagua Abdur Rahmaan bin Auf (Radhiyallahu ‘anhu) Kama kiongozi wa jeshi na kwa hivyo alimwambia Bilaal (Radhiyallahu’ Anhu) kumkabidhi bendera kwake. Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) kisha akamdhukuru Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah), akajisalimia mwenyewe, na akasema:

“Ewe ibnu auf, chukua bendera, na nenda katika njia ya Mwenyezi Mungu pamoja na Jeshi. Pigana na watu hao ambao hawamuamini Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah). Usiibe ngawira za vita, usiende kinyume na ahadi zako (ambayo umefanya na madui), usikate kate miili ya madui, na usiwauwe watoto. Hii ndio amri ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) na njia ya Nabi wake (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) ambayo imekukujia. ”

Baada ya hapo, Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alimtuma katika njia ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) na
Jeshi la wanaume mia saba kuelekea kabila la Kalb, lililoko katika eneo linaloitwa Dumat al-Jandal. Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) kisha akampa ushauri ufuatao akisema:

“Ikiwa watu wa sehemu hio wanaokubali (Uislamu), basi unapaswa kumuoa binti wa kiongozi wao.”

Abdur Rahmaan (Radhiyallahu ‘Anhu) kwa hivyo aliondoka na jeshi lake hadi alipowafikia Watu wa Dumat al-Jandal. Alibaki hapo kwa siku tatu, akiwapa da’wa kuukubali Uislamu.

Siku ya tatu, kiongozi wa Dumat al-Jandal, Asbagh, ambaye alikuwa Mkristo, alikubali Uislam. Watu wengine kutoka kabila lake pia walikubali Uislamu. Wale ambao walichagua kutokukubali Uislamu walikubali kulipa Jizyah.

Abdur Rahmaan (Radhiyallahu ‘Anhu) kisha akaandika barua kwa Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi Wasallam) akimjulisha juu ya hali hiyo na kuthibitisha tena ikiwa anapaswa kumuoa binti wa kiongozi wao. Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alijibu barua yake akisema kwamba anapaswa kwenda mbele na kuolewa na binti ya kiongozi, Asbagh. Abdur Rahmaan (Radhiyallahu ‘Anhu) kwa hivyo aliolewa na binti yake ambaye jina lake alikuwa Tumaadhir (Radhiyallahu’ Anha). (Bazzaar #6175, Majma’uz Zawaid #9615, Sharh Zurqani 3/133)

About admin

Check Also

Abdur-Rahman bin Awf (Radhiya Allaahu ‘anhu) Akiongoza Swalaah.

Wakati wa safari ya Tabook, Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) walikuwa wakisafiri pamoja na Rasulullah (Sallallahu …