Damu Ya Kwanza iliyomwagika kwa ajili ya Uislamu

Muhammad bin Ishaaq (rahimahullah) anasimulia:

Mwanzoni katika Uislamu, Maswahaabah wa Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) walikuwa wakiswali kwa siri. Walikuwa wakienda kwenye mabonde ya Makka Mukarramah kuswali ili Swalah zao zibaki siri kwa makafiri (na ili waokoke na mateso ya makafiri).

Wakati mmoja, wakati Sa’d (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwepo pamoja na kundi la Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) wakiswali katika moja ya mabonde ya Makkah Mukarramah, kundi la makafiri liliwaona. Kisha makafiri wakaanza kuwachokoza na kutukana Dini yao, mpaka ukazuka ugomvi baina ya makundi mawili (yaani Maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) na makafiri). Wakati wa ugomvi huu, Sa’d (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimumiza vibaya kafiri mmoja kichwani kwa kumpiga fuvu la kichwa na mfupa wa taya ya ngamia. Haya yalikuwa ni mapambano ya kwanza (yaliyotokea tangu mwanzo wa Uislamu ambapo Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) walisababisha majeraha ya kimwili kwa makafiri na yalikuwa ni ugomvi) ambayo damu ilimwagwa kwa ajili ya Uislamu. (Usdul Ghaabah 2/308)

About admin

Check Also

Upendo Kwa Answaar

‘Aamir (rahimahullah), mtoto wa Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu), anasimulia yafuatayo: Wakati fulani nilimwambia baba yangu, …