عن عائشة قالت قال رسول الله صلى الله عليه وسلم من سره أن يلقى الله وهو عليه راض فليكثر الصلاة علي (الكامل في ضعفاء الرجال ٦/٣٢، وإسناده ضعيف كما في القول البديع صـ ٢٦٧)
Sayyidatuna Aisha (radhiyallahu ‘anha) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaihi Wasallam) amesema, “yoyote anayetaka kukutana na Allah subhaana wata’alah katika hali Allah subhaana wata’alah yupo radhi naye inabidi anisalie mimi kwa wingi.”
Kuwapa Upendeleo majirani wa Rasulullah (sallallahu alaihi Wasallam)
Imam Malik (rahimahullah) alikuwa akianza kuwafundisha wanafunzi wa Hadith na wale waliokuwa wakiishi Madinah Munawwarah kabla ya kufundisha wengine. Alipoulizwa sababu ya kuwapendelea wanafunzi wa Hadith na watu wa Madinah, alisema: “Hawa ni majirani wa Rasulullah”.