Mapenzi Makubwa ya Maswahaba (radhiyallahu ‘anhum) kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Siku moja, mtu mmoja alikuja kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na akasema: “Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) mapenzi yangu kwako ni kwamba ninapokufikiria wewe huzidiwa na mapenzi yako, kiasi kwamba sipati kuridhika mpaka nikuone. Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), mawazo yananipitia moyoni mwangu kwamba ikiwa Allah ta’ala atanijaalia Pepo, itakuwa vigumu sana kwangu kukuona, kwa sababu utakuwa katika nafasi ya juu ambapo sitaweza kufika (vipi nitawezaje kuishi bila wewe).”

Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akamtuliza kwa kumsomea aya ifuatayo katika jibu lake.

وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ فَأُو۟لَٰٓئِكَ مَعَ ٱلَّذِينَ أَنْعَمَ ٱللَّهُ عَلَيْهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّنَ وَٱلصِّدِّيقِينَ وَٱلشُّهَدَآءِ وَٱلصَّٰلِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُو۟لَٰٓئِكَ رَفِيقًا ‎﴿٦٩﴾‏

Watu wote wanaomtii Allah subhaana wata’ala na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) wamo katika kundi la wale ambao juu yao ziko rehema za Allah ta’ala; Manabii, Siddiqin, Mashahidi, na Wachamungu.

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …