Sunna Na Adabu Za Dhul Hijjah 3

5. Ni Mustahab kwa mtu (ambaye hayuko katika Ihraam) kufunga siku ya Arafah yaani 9 ya Dhul Hijjah. Mbali na kupokea thawabu ya mwaka mmoja, dhambi za miaka miwili pia zitasamehewa.

Abu Qataadah(Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Sahaabi mmoja aliwahi kumuuliza Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam), “Ewe Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam), mtu anayefunga siku ya Aashuraa atapata malipo gani?” Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akajibu, “atapata thawabu ya kufunga mwaka mzima. ” Sahaabi kisha akauliza, “Je! Ni malipo gani mtu atatpata akifunga siku ya arafah, rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akajibu, “Inafuta madhambi (ndogo ndogo) za mwaka huu na mwaka uliopita.”[1]

Ibnu Umar (Radhiyallahu anhuma) anaripoti kwamba, “Niliwahi kuhiji na Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) na Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akufunga Siku ya Arafah (wakati wa Hajj). Nikahiji na Abu Bakr (Radhiyallahu anhu) na yeye pia hakufunga siku ya Arafah (wakati wa Hajj). Hivyo hivyo, nikahiji na Umar (Radhiyallahu anhu), na yeye pia hakufunga siku ya Arafah (wakati wa Hajj), na kisha nikahiji na Uthmaan (Radhiyallahu anhu), na yeye hakufunga siku ya Arafah (wakati wa Hajj). “[2]

6. Siku ya Arafah, soma dua ifuatayo kwa wingi:

لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيْكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ بِيَدِهِ الْخَيْرُ وَهُوَ عَلٰى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيْرٌ

Hakuna mungu apasaye kuabudiwa isipokuwa Allah Ta’ala, ambaye hana mwenzi. Kwake ni ufalme (wa ulimwengu wote), na kwake yeye ni sifa zote. Katika mikono yake (udhibiti) peke yake ni mazuri yote na yeye peke yake ana nguvu kamili juu ya kila kitu.[3]


[1] صحيح ابن حبان، الرقم: 3631

[2] سنن الترمذي، الرقم: 750، وقال: هذا حديث حسن

[3] مسند أحمد، الرقم: 7080، و قال العلامة الهيثمي رحمه الله في مجمع الزوائد، الرقم: 5550، رواه أحمد ورجاله موثقون

About admin