Monthly Archives: June 2022

Kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) kabla ya Kufanya Dua

Fadhaalah bin Ubaid (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba katika tukio moja, pindi Rasulullah sallallahu alaihi wasallam alikuwa amekaa (msikitini), mtu fulani aliingia na kuswali. Baada ya kuswali, mtu huyo aliomba dua akisema, “Ewe Allah subhaana wata'ala! Nisamehe na unimiminie rehema zako!” kumtazama namna mtu huyu alivyoomba dua, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akamwambia: “Umeharakisha (kumwomba Allah ta'ala haja yako), Ewe Mtu aliye swali! Baada ya kuswali, unapokaa kufanya dua, anza kwa kumhimidi Allah (subhaana wata'ala) kwa vile anastahiki kusifiwa. Baada ya hapo nitumie mimi salaa na salaam, kisha mletee Allah ta'ala haja yako.” Baada ya hapo, mwingine mtu aliyeswali. Baada ya kuswali, alimhimidi Allah (subhaana wata'ala), akamtumia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) salaa na salaam (na kisha akaanza kuomba). Kumwangalia mtu huyu (na yeye akishikamana na adabu za dua), Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akamwambia, “Ewe mtu aliye swali! Omba dua, kwa sababu dua yako itakubaliwa!”

Soma Zaidi »