Hazrat Abdur Rahmaan Bin Auf (radhiyallahu 'anhu) alitowa taarifa kuwa kuna wakati mmoja, nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) alitoka nyumbani kwake na mimi nikamfuata, mpaka akaingia kwenye shamba la tende na hakashuka chini kusujudu. Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) alifanya sajida ndefu mpaka ni kaogopa kuwa mwenyezi mungu tayari amesha mchukuwa.
Soma Zaidi »Njia Za Suna Za Kufanya Udhu – Sehemu Ya Pili
4. Osha mikono yote mpaka kwenye vifundo mara tatu
Sayyidina Humraan (rahimahullah), mtumwa aliye huru wa Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kuwa Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu)aliomba aletewe maji (kuonyesha watu jinsi gani ya kuchukuwa udhu). Kisha alianza kutawadha kwa kuosha mikono (mpaka kwenye vifundo) mara tatu. (kwenye riwaya hii, iliyopatikana ndani ya Sahihi Bukhari, Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) kasema ” nilimuona Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wassallam) anafanya udhu kwa namna hii.)”
Soma Zaidi »Njia Za Suna Za Kufanya Udhu – Sehemu Ya Kwanza
1. Pindi hukifanya udhu, elekea qibla na kaa sehemu ya juu ( mf: kiti) ili usipatwe na maji yaliyotumika. Sehemu ambayo mtu anafanya udhu iwe safi.
Sayyidina Abd kheir (rahimahullah) ameripoti kwamba kiti kililetwa kwa Sayyidina Ally (radhiyallahu ‘anhu). Kisha aka kaa juu ya kiti ( kwa ajili ya kuonyesha udhu wa Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam).
Soma Zaidi »Masaili Ya Kawaida Yanayohusiana Na Kujisaidia Mwenyewe
1. S: Je inaruhusiwa kusoma kitu chochote kilichoandikwa kwa mfano magazet,kutumia simu kuchat, kutumia internet, na mengineyo wakati uko chooni ?
J: Chooni ni sehemu ambayo mtu anajisaidia, hivyo haipendezi kwa mtu kutumia simu yake au kusoma kitu chochote chenye maandishi chooni.[1]
Soma Zaidi »Aina Za Sunna Za Kufanya Istinja – Saheemu Ya saba
22. Pindi ukitumia choo Usikiache katika hali ya uchafu mf: kuchafua juu ya choo au kuchafua chini, kwa kutofurashi na maji nk:kama unatumia choo ambacho kinatumiwa na watu wengine kuwa makini zaidi kwa utumiaji wako ili usilete usumbufu kwao
Soma Zaidi »Aina Za Sunna Za Kufanya Istinja – Saheemu Ya Sita
20. Toka chooni na mguu wa kulia na mshukuru Allah subhaana wata'alah kwa kuruhusu machafu kutoka mwilini na kukujalia kukupa mazuri ya afya. Njia ya kumshukuru Allah subhaana wata'alah ni kusoma dua ifuatayo ukiwa unatoka chooni baada ya kujisaidia
Soma Zaidi »Aina Za Sunna Za Kufanya Istinja – Saheemu Ya Tano
17. Chukuwa tahadhari sana kuhakikisha kuwa hupatwi na cheche za mkojo mwilini. Hukifanya uzembe kwa hili kuna adhabu kaburini.
Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) alisema kuwa mtume (sallallahu ‘alaihi wassallam) amesema ” adhabu kali (zitakazo wakabili watu wengi) kaburini ni adhabu za mkojo (mf: mtu kutokuwa makini kwa cheche za mkojo ambazo zinampata. Kwa ajili ya hilo udhu, sala zao na ibada zingine hazitokubalika kwa kuwa mtu anakuwa mchafu”)
Soma Zaidi »Aina Za Sunna Za Kufanya Istinja – Saheemu Ya Nne
11. Usizungumze ukiwa unajisaidia, labda kuwe na shida muhimu wa kuongea.
Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu 'anhu) alitowa taarifa kuwa Nabii wa Allah subhaana wata'alah (sallallahu 'alaihi wassallam) amesema "watu wawili wasiende pamoja kujisaidia sehemu moja na kuongea pamoja wakiwa watupu (yaani sehemu zao za siri) ziko wazi kwa hakika mwenyezi mungu hapendi kitendo hicho.
Soma Zaidi »Aina Za Sunna Za Kufanya Istinja – Saheemu Ya Tatu
7. Ingia chooni na mguu wako wa kushoto
8. Usivuwe nguo yako ukiwa umesimama anza kuvua nguo yako ukiwa umekaribia chini hili utumie muda mchache kwa kufunua sehemu zako za siri.
Sayyidina Abdullah Bin Umar (radhiyallahu 'anhuma) ametowa ripoti kuwa pindi Nabii wa Allah subhaana wata'alah (sallallahu 'alaihi wassallam) alipokuwa anataka kujisaidia alikuwa hapandishi nguo yake mpaka akaribie kufika chini.
Soma Zaidi »Aina Za Sunna Za Kufanya Istinja – Saheemu Ya Pili
4. Jifunike kichwa na uvae viatu kabla hujaingia chooni.
Sayyidina Habeeb Bin Saalih(rahimahullah) alitowa taarifa kuwa Nabii wa Allah subhaana wata'alah (sallallahu 'alaihi wassallam) alikuwa ana vaa viatu na anajifunika kichwa chake cha baraka wakati akiingia chooni.
Soma Zaidi »