Habbaan Bin Munqiz (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba sahabi moja aliwahi kumuuliza Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam), "Ewe mjumbe wa Allah (sallallahu alaih wasallam) je nijitolee thuluthi moja ya muda ambao nimezitenga kufanya dua ili nitume salaam kwako? "Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) Alijibu, "ndio, kama utapenda." Ule sahabah akauliza, "je nijitolee thuluthi mbili ya muda ambao nimezitenga kufanya dua ili nitume salaam kwako? "Nabii wa allah akajibu tena, "ndio, kama utapenda. "ule sahabah akauliza, "je nijitolee muda wote kukutumia salaam? "Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) akajibu, "kama utafanya hivyo, Allah subhaana wata'alah Atayatimiza mahitaji yako yote ambayo unayo (na amboyo ungeulizia kwenye dua yako), ikiwa niyakuhusu dunia au aakhera."
Soma Zaidi »