Faradhi Za Ghusl Kuna matendo mawili ya faradhi kwenye ghusl 1. Kuweka niyyah ya kufanya ghusl kabla ya kuanza kuosha mwili 2. Kumimina maji mwili mzima.[1] Sunna Za Ghusl Matendo ya sunna kwenye ghusl 1. Kusoma tasmiyah mwanzoni mwa ghusl.[2] 2. Kuosha mikono mpaka kwenye vifundo.[3] 3. Kuosha sehemu za …
Soma Zaidi »Kukubalika Kwa Dua
Imepokelewa kutoka kwa Umar (radhiallahu anhu) dua zinabaki zimesimamishwa kati ya mbigu na ardhi. Hazitafika mbinguni Kama salaam haijatumwa kwa Nabii (sallallahu alaihi wasallam) (yaani hakuna uwakika wa kukubalika)."
Soma Zaidi »Njia Za Sunna Za Kufanya Ghusl- Sehemu Ya Tano
16.usijeshughulishe na kuongea, au kuimba au mazungumzo yoyote pindi utakapokuwa unafanya ghusl.
17. Usitumiye muda mwingi bafuni haswa kama bafu yenyewe inatumiwa na watu wengine.
18. Usichafuwe bafu na nywele ulizo nyowa.
Soma Zaidi »Ongezeko la rizki
Sahl bin Sa'd (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba kuna wakati mmoja, sahaba mmoja alimfata Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) Na akalalamika juu ya umasikini na ugumu wa kupata rizki. Nabi wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akamuambia huyu sahaba, "pindi unapo ingia nyumbani kwako, kuwepo watu ndani au hata kama hamna watu ndani basi toa salaam. Baada ya hapo nitumie mimi salaam na soma Qul-Huwallah (surah ikhlaas) mara moja". Sahaba akafanya jinsi alivyo amrishwa na Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam), na Allah subhaana wata'alah akambariki kwa utajiri mwingi na akaanza kutumia kwa majirani na ndugu zake.
Soma Zaidi »Njia Za Sunna Za Kufanya Ghusl- Sehemu Ya Nne
13. Mimina maji mwilini upande wakulia kutoka juu ya mwili mpaka chini mara tatu, baada ya hapo mimina maji mwilini upande wa kushoto kutoka juu ya mwili mpaka chini mara tatu. Sunnah itakua imetimizwa kwa kuosha mwili kwa njia hii. Pia ni sahihi kuosha upande wa kulia mara moja , …
Soma Zaidi »Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama
Ibnu umar (radhiyallahu anhuma) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) Alisema, "Pamba mikusanyiko yenu na kunitumia salaam, kwa sababu siku ya qiyaama, salamu zenu juu yangu itakuwa nuru (sababu ya nuru) kwenu."
Soma Zaidi »Njia Za Sunna Za Kufanya Ghusl- Sehemu Ya Tatu
9. Fanya udhu uliyo kamilika.
Sayyidatuna Aaisha (radhiyallahu anha) ameripoti kwamba pindi Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) alikuwa akitaka kufanya ghusl ya fardh, alikuwa akianza kwa kuosha mikono yake ya barakah kabla ya kuziingiza ndani ya kopo la maji. Alafu alikuwa akiosha sehemu zake za siri na kufanya udhu , kama jinsi anavyofanya udhu wa swala."
Soma Zaidi »Thawabu ya sadaqa kupitia kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam)
Abu sa'eed khudri (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) amesema, muislamu yoyote ambaye hana chochote kutoa kama sadaqa, inabidi amtumie Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) hii salaam kwenye dua yake kwa sababu ni njia ya yeye kupata thawabu ya sadaqa na itamsafishia madhambi zake."
Soma Zaidi »Njia Za Sunna Za Kufanya Ghusl – Sehemu Ya Pili
4. Kama unafanya ghusl ndani ya shawa basi hakikisha autumii maji vibaya. Usijishughulishe na kupaka sabuni au kunyowa nywele zisizohitajika (mf: makwapani na sehemu za siri) wakati bomba la maji lipo wazi. Huu ni uharibifu mkubwa na nisababu ya kupata madhambi
Soma Zaidi »Kupokea Cheti cha Uhuru kutokana na Unafiki na moto wa Jahannam
Anas (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) amesema, "yoyote atakae nitumia salaam mara moja, kwa kumlipa Allah subhaana wata'alah atamtumia salamu mara kumi (yaani: ataampa zawadi na atamfariji na rehma zake), na yoyote atakae nitumia salaam mara kumi, Allah subhaana wata'alah atamtumia salaam mara mia (yaani: ataampa zawadi na atamfariji na rehma zake), na yoyote atakae nitumia salaam mara mia, Allah subhaana wata'alah Atamwandikia (cheti) uhuru, katikati ya macho yake mawili, kutokana na unafiki, (na cheti ya) uhuru kutokana na moto wa jahannum, na Allah subhaana wata'alah ataampa heshma na faraja ya kuwa na mashahidi siku ya qiyamah."
Soma Zaidi »