Dhul hijjah

Zul Hijjah ni miongoni ya miezi minne takatifu ndani ya kalenda ya Kiisilamu. Miezi minne takatifu ni Dhul Qa’dah, Dhul Hijjah, Muharram na Rajab. Thawabu za matendo mema yatakayofanywa katika hizi miezi zitaongezeka, na dhambi zilizofanywa katika miezi hizi
pia huhesabiwa kuwa mabaya zaidi. Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) anasema:

إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللَّهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللَّهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ

Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Mwenyezi Mungu tangu alipo umba mbingu na ardhi. Ndani ya hizo minne mitakatifu.

Ukubwa wa siku kumi za kwanza na usiku wa dhul hijjah zinaweza kuzingatiwa kwamba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) alichukua kiapo kwenye usiku wa kwanza wa dhul Hijjah katika Quraan Majeed, na fadhila maalum zimerekodiwa katika Ahaadith ya Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) kuhusu siku hizi. Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) anasema:

وَالْفَجْرِ ‎﴿١﴾‏ وَلَيَالٍ عَشْرٍ ‎﴿٢﴾‏

Naapa kwa mwangaza wa asubuhi unapo ufukuza usiku na kwa masiku kumi (za dhul hijjah)

Sunna na Aadaab za Dhul Hijjah

1. Jitahidi kujishughulisha na Ibaadah katika siku kumi za kwanza za dhul hijjah. Thawabu kubwa zimetajwa kuhusu Ibaadah itakayofanywa katika siku hizi kumi.

Abdullah bin Abbaas (Radhiyallahu anhuma) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Hakuna matendo mazuri iliyofanywa katika siku yoyote ndani ya mwaka ambayo ni nzuri zaidi kuliko matendo mazuri itakayofanywa katika siku hizi kumi za dhul Hijjah.” Maswahaabah (Radhiyallahu anhum) wakauliza, “Hata Jihaad?” Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akajibu, “Hata Jihaad, isipokuwa kwa yule anayehatarisha maisha yake na utajiri (katika Jihaad) na harudi na chochote (yaani Jihaad iliofanywa ndani ya hizi siku kumi za dhul hijjah ni bora zaidi kuliko jihaad Muda wowote mwingine ule ndani ya mwaka, isipokuwa Jihaad ya Mujaahid ambaye anakuwa shahidi). “[1]

2. Jaribu kufunga ndani ya siku kumi za kwanza. Kwa kufunga siku yoyote ndani ya siku kumi za kwanza za Dhul Hijjah (kutoa siku ya kumi), utapokea thawabu ya kufunga mwaka mzima.[2]


[1] صحيح البخاري، الرقم: 969

[2 ويستحب صوم تسعة أيام من أول ذي الحجة كذا في السراج الوهاج (الفتاوى الهندية 1/201)

About admin

Check Also

Fadhila za Jumu’ah 2

Siku Ambayo Ina Muda Maalum wa Kukubalika Anas bin Maalik (radhiyallahu anhu) anaripoti: Siku ya …