Sunna na Aadaab za Jumu’ah 3

9. Ikiwezekana, kwenda msikitini kwa kutembea kuswali Jumu’ah. Kwa kila Hatua zitazochukuliwa, utapokea thawabu ya kufunga mwaka mmoja na kuswali Tahajjud kwa mwaka mmoja.

Aws bin aws thaqafi (radhiallahu anhu) anasema, “Nilimsikia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akitaja, ‘Yule anayefanya ghusl siku ya Jumuah na anaenda mapema msikitini kwa kutembea, na haendi kwa kutumia usafiri, na anakaa karibu na Imaam na husikiliza khutbah kwa makini, na hashiriki katika shughuli yoyote, kwake yeye atapata thawabu ya kufunga kwa mwaka mmoja na kusimama katika Tahajjud kwa kila hatua anayoichukua wakati akienda msikitini.’”[1]

10. Sikiliza Khutbah kwa umakini, hata kama huelewi. Usizungumze wala kuwambie wengine kukaa kimya wakati khutbah inatolewa.[2]

Ibnu Abbaas anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Mfano wa yule anayeongea siku ya Jumu’ah wakati Imaam akitoa Khutbah ni sawa sawa na punda anaye beba mzigo wa vitabu mgongoni mwake (yaani Kama vile punda aliyebeba mzigo wa vitabu vya Deeni mgongoni mwake hafaidika na vitabu vya Deeni, hivyo ndivyo yule atakayeongea wakati Khutbah inatolewa hatopata faida yoyote). Na yule ambaye anamwambia mwingine abaki kimya (wakati khutbah Inatolewa), hakuna Jumu’ah kwake. (i.e. ingawa anamshauri mwingine abaki kimya wakati wa khutbah, yeye mwenyewe amefanya dhambi kutokana na kuongea wakati Khutbah inaendelea). “[3]

11. Mswalie Mtume (sallallahu alaihi wasallam) kwa wingi.

Aws bin aws (radhiallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Siku bora zaidi ni siku ya Jumu’ah. Kwa hivyo, nitumieni swala na salaam siku hio, hakika swala na salaam zenu zinanifikia.”[4]


[1] سنن أبي داود، الرقم: 345، مسند أحمد، الرقم: 6954، وقال العلامة المنذري رحمه الله في الترغيب والترهيب، الرقم: 1036: رواه أحمد ورجاله رجال الصحيح

[2] عن أبى هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: إذا قلت لصاحبك يوم الجمعة: أنصت والإمام يخطب فقد لغوت (صحيح البخاري، الرقم: 934)

(وكل ما حرم في الصلاة حرم فيها) أي في الخطبة خلاصة وغيرها فيحرم أكل وشرب وكلام ولو تسبيحا أو رد سلام أو أمرا بمعروف بل يجب عليه أن يستمع ويسكت (الدر المختار 2/159)

[3] مسند أحمد، الرقم: 2033، وقال العلامة الهيثمي رحمه الله في مجمع الزوائد، الرقم: 3123: رواه أحمد والبزار والطبراني في الكبير وفيه مجالد بن سعيد وقد ضعفه الناس ووثقه النسائي في رواية

About admin

Check Also

Fadhila za Jumu’ah

Kusamehewa Madhambi Kwa Kuswali Jumu’ah Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu …