{"id":3592,"date":"2026-08-12T07:04:21","date_gmt":"2026-08-12T05:04:21","guid":{"rendered":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3592"},"modified":"2026-08-12T11:43:00","modified_gmt":"2026-08-12T09:43:00","slug":"uhusiano-wa-karibu-ambao-muaaz-bin-jabal-radhiya-allaahu-anhu-alifurahia-na-rasulullah-sallallahu-alaihi-wasallam","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3592","title":{"rendered":"Uhusiano wa Karibu Ambao Mu\u2019aaz bin Jabal (Radhiya Allaahu \u2018anhu)\u00a0Alifurahia na Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam)"},"content":{"rendered":"<p><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" class=\"alignnone wp-image-3595 size-full\" src=\"https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2026\/08\/Swahili_158_9.jpg\" alt=\"\" width=\"1080\" height=\"1080\" srcset=\"https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2026\/08\/Swahili_158_9.jpg 1080w, https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2026\/08\/Swahili_158_9-300x300.jpg 300w, https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2026\/08\/Swahili_158_9-1024x1024.jpg 1024w, https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2026\/08\/Swahili_158_9-150x150.jpg 150w, https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2026\/08\/Swahili_158_9-768x768.jpg 768w, https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2026\/08\/Swahili_158_9-200x200.jpg 200w\" sizes=\"auto, (max-width: 1080px) 100vw, 1080px\" \/><\/p>\n<p>Muaz bin Jabal (Radhiya Allaahu \u2018anhu) ametaja, \u201cWakati mmoja, nilikaa nyuma ya Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) juu ya punda alipokuwa amempanda. Hapakuwa na kitu baina yangu na Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) zaidi ya mbao la tandiko (ambalo humtenganisha mpanda farasi na aliyekaa nyuma yake).<\/p>\n<p>\u201cMtume (Sallallahu alaihi wasallam) alinihutubia akisema, \u2018Ewe Mu\u2019aaz!\u2019 Nikamjibu, \u2018Mimi nipo katika utumishi wako, ewe Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam).<\/p>\n<p>\u201cMtume (Sallallahu alaihi wasallam) alikaa kimya na akaendelea kumpanda mnyama huyo. Baada ya muda kidogo, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akaniambia tena akisema, \u2018Ewe Mu\u2019aaz!\u2019 Nikamjibu, \u2018Nipo katika utumishi wako ewe Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam).<\/p>\n<p>\u201cBaada ya muda kidogo kupita, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alinihutubia kwa mara ya tatu akisema, \u2018Ewe Mu\u2019aaz!\u2019 Nikamjibu, \u2018Mimi nipo katika utumishi wako, ewe Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam).<\/p>\n<p>\u201cMtume (Sallallahu alaihi wasallam) akaniambia, \u2018Je, unajua haki ya Allah Ta\u2019ala juu ya waja Wake?<\/p>\n<p>\u201cNikajibu, \u2018Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (Sallallahu alaihi wasallam) wanajua zaidi (yaani mimi sijui).<\/p>\n<p>\u201cMtume (Sallallahu alaihi wasallam) akasema, \u2018Haki ya Allah Ta\u2019ala juu ya waja Wake ni kumuabudu Yeye bila ya kumshirikisha (yaani. watekeleze ibada zote kwa ajili ya radhi yake tu na waendelee kuwa watiifu kwake kila wakati, huku wakijiepusha na kumuaasi).<\/p>\n<p>\u201cBaada ya hapo, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) aliendelea kumpanda mnyama huyo na akanyamaza kwa muda kidogo. Baada ya muda kidogo kupita, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akanihutubia tena akisema, \u2018Ewe Mu\u2019aaz!\u2019 Nikamjibu, \u2018Nipo katika utumishi wako, ewe Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam).<\/p>\n<p>\u201cMtume (Sallallahu alaihi wasallam) akaniambia: \u2018Je, unajua haki ya waja juu ya Allah Ta\u2019ala ikiwa wanatekeleza Aliyowaamrisha kuyafanya (yaani ni haki gani ya waja juu ya Allah Ta\u2019ala ikiwa wanatekeleza ibada zote kwa ajili ya radhi Yake tu na wakabaki wakimtii Yeye kila wakati, huku wakijiepusha na kumuaasi)?\u2019<\/p>\n<p>\u201cNikajibu, \u2018Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (Sallallahu alaihi wasallam) wanajua zaidi (yaani mimi sijui).<\/p>\n<p>\u201cMtume (Sallallahu alaihi wasallam) akaniambia: \u2018Haki ya waja juu ya Allah Ta\u2019ala ni kwamba Allah Hawaadhibu na Anawaingiza Jannah (yaani. ikiwa waja wataendelea kuwa watiifu kwa Allah Ta\u2019ala wakati wote huku wakijiepusha na uasi wake, basi Allah Ta\u2019ala hatowaadhibu waja wake kwa kuwaingiza Jahannamu bali atawabariki kwa rehema zake na kuwaingiza Jannah).\u2019\u201d<\/p>\n<p>Kutokana na tukio hili, tunaona uhusiano wa karibu\u00a0ambao Mu\u2019aaz bin Jabal (Radhiyallahu\u00a0\u2018anhu) alifurahia na Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam).<\/p>\n<p>Sababu ya Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) kukaa kimya mara tatu baada ya kumhutubia Muaaz (Radhiya Allaahu \u2018anhu) ilikuwa ni kujenga shauku ndani yake ya kusikia kile ambacho Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) anakwenda kumfundisha. Kwa vile suala ambalo Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alitaka kumfundisha lilikuwa na umuhimu mkubwa, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alichukua njia hii alipokuwa akizungumza naye.<\/p>\n<p>Vile vile tunaona heshima ya hali ya juu ambayo Muaz (Radhiya Allaahu \u2018anhu) alionyesha kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alipokuwa akizungumza naye.<\/p>\n<p>Muaaz (Radhiya Allaahu \u2018anhu) alimjibu Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) kwa shauku moja mara tatu zote ambazo Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alizungumza naye.<\/p>\n<p>(Sahih\u00a0Bukhari\u00a0#6500,\u00a0Sahih\u00a0Muslim #30,\u00a0Fathul\u00a0Baari\u00a011\/339)<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Muaz bin Jabal (Radhiya Allaahu \u2018anhu) ametaja, \u201cWakati mmoja, nilikaa nyuma ya Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) juu ya punda alipokuwa amempanda. Hapakuwa na kitu baina yangu na Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) zaidi ya mbao la tandiko (ambalo humtenganisha mpanda farasi na aliyekaa nyuma yake). \u201cMtume (Sallallahu alaihi wasallam) alinihutubia akisema, \u2018Ewe Mu\u2019aaz!\u2019 Nikamjibu, \u2018Mimi nipo &hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":4,"featured_media":3595,"comment_status":"closed","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[25],"tags":[],"class_list":["post-3592","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","","category-sahaabah"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3592","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/4"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=3592"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3592\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3596,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3592\/revisions\/3596"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/3595"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=3592"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=3592"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=3592"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}