{"id":3578,"date":"2026-07-29T11:50:39","date_gmt":"2026-07-29T09:50:39","guid":{"rendered":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3578"},"modified":"2026-08-06T08:18:05","modified_gmt":"2026-08-06T06:18:05","slug":"kuthamini-baraka-ya-maisha","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3578","title":{"rendered":"Kuthamini Baraka ya Maisha"},"content":{"rendered":"<p>Dawood bin Dinaar (rahimahullah) alikuwa Imaam mkubwa katika fani ya Hadithi na mwalimu wa Muhadditheen mashuhuri, mfano wa Imaam Shu\u2019bah ( rahimahullah) na Imaam Wakee\u2019 (rahimahullah).<\/p>\n<p>Wakati wa uhai wake, tauni ilikuwepo eneo la Khuraasaan alipokuwa akiishi. Kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa wameugua wakati wa tauni na wengi walipoteza maisha.<\/p>\n<p>Dawood bin Dinaar (rahimahullah) alikuwa miongoni mwa wale waliopatwa na tauni na kuugua. Hata hivyo, kwa vile Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) hakumuandikia kifo wakati huo, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) alimbariki na shifaa kutokana na tauni na akaufanya ugonjwa huu kuwa njia ya mafanikiyo yake ya kiroho.<\/p>\n<p>Anaripoti kwamba katika kipindi cha ugonjwa wake, mara moja alianguka na kupoteza fahamu, na katika hali hii, alionyeshwa maono ambayo paa la nyumba yake lilipasuka na malaika wawili walishuka juu yake kutoka mbinguni.<\/p>\n<p>Malaika mmoja aliketi karibu na kichwa chake, na mwingine akaketi miguuni kwake. Malaika aliyeketi karibu na miguu yake akaanza kuzichunguza nyayo za miguu yake, huku malaika aliyeketi kwenye ubavu wa kichwa chake akifungua kinywa chake na kuuchunguza ulimi wake na sehemu ya ndani ya kinywa chake.<\/p>\n<p>Malaika aliyeichunguza miguu yake alimjulisha malaika aliyeketi karibu naye upande wa kichwa, &#8220;Nimegundua kwamba mara nyingi hutumia miguu hii kutembea kwenda msikitini kwa ajili ya swalah.&#8221;<\/p>\n<p>Kwa maneno mengine, malaika alikuwa akionyesha kwamba yeye ni miongoni mwa hao wanaokwenda Msikitini kwa ajili ya Swalah na kupata malipo makubwa yaliyotajwa ndani yaa hadith kwa wale wanaokwenda Msikitini &#8211; kwamba kwa kila hatua wanayoichukua, huandikwa wema mmoja, hupandishwa daraja moja na kufutiwa dhambi moja kwenye kitabu cha matendo yao.<\/p>\n<p>Malaika akiuchunguza ulimi na mdomo wake kisha akamfahamisha malaika alikuwa ameketi miguuni kwake, \u201cNimeona ulimi na kinywa chake kuwa na alama ya kusoma tahmid (kusoma Alhamdulillah), tasbihi (kusoma Subhanallah) na dhikr ya Allah Ta\u2019ala. Hata hivyo, naona kwamba usomaji wake wa Quran Majeed ni mdogo.\u201d<\/p>\n<p>Kwa maneno mengine, malaika alikuwa akionyesha kwamba licha ya Dawood bin Dinaar (rahimahullah) kuwa miongoni mwa Muhadditheen wa ngazi ya juu wa zama zake, na akijishughulisha na huduma ya Hadith, kitu kilichokosekana katika maisha yake kilikuwa ni kisomo cha Quraan Majeed. Kwa hiyo, alikuwa akifahamishwa udhaifu wake kupitia malaika.<\/p>\n<p>Baada ya hapo, malaika mmoja akamwambia mwenzake, \u201cWakati wake wa kuondoka katika ulimwengu huu bado haujafika.\u201d Akisema hivyo, paa la nyumba yake likafunguka na wale malaika wawili wakaondoka, na kisha paa likafungwa tena.<\/p>\n<p>Baada ya kupata fahamu, Dawood bin Dinaar (rahimahullah) alitambua kwamba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) amembariki kwa nafasi ya uzima ili kurekebisha udhaifu wake. Hivyo alianza kusoma Qur-aan Majeed kwa wingi na pia akajishughulisha na kuipata elimu mbalimbali zinazohusiana na Quraan Majeed.<\/p>\n<p>Kutokana na tukio hili, tunaelewa kwamba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) anapotaka kumbariki mja, basi kwa njia za kipekee na za mafumbo, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) humjulisha udhaifu wake na humpa tawfeeq ya kurekebisha maisha yake.<\/p>\n<p><strong>Kujihusisha na Utambuzi wa Kila Siku<\/strong><\/p>\n<p>Tunafundishwa katika Hadith kwamba tunapoamka, tunanapaswa kusoma dua ya masnoon:<\/p>\n<p class=\"\" dir=\"RTL\" style=\"text-align: center; font-family: 'Traditional Arabic'; font-size: 16pt;\">\u0627\u064e\u0644\u0652\u062d\u064e\u0645\u0652\u062f\u064f \u0644\u0650\u0644\u0651\u0670\u0647\u0650 \u0627\u0644\u0651\u064e\u0630\u0650\u064a\u0652 \u0623\u064e\u062d\u0652\u064a\u064e\u0627\u0646\u064e\u0627 \u0628\u064e\u0639\u0652\u062f\u064e \u0645\u064e\u0627 \u0623\u064e\u0645\u064e\u0627\u062a\u064e\u0646\u064e\u0627 \u0648\u064e\u0625\u0650\u0644\u064e\u064a\u0652\u0647\u0650 \u0627\u0644\u0646\u0651\u064f\u0634\u064f\u0648\u0652\u0631\u0652<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><em>Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyetujaalia uhai baada ya kufa na kwake Yeye tu ndio tutarejeshwa.<\/em><\/p>\n<p>Katika dua hii, tunakumbushwa kwamba kila kikikucha, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) Anatubariki na fursa nyingine ya maisha na nafasi ya kurekebisha maisha yetu na kuweka mambo yetu sawa kabla ya muda wetu hapa duniani kuisha.<\/p>\n<p>Kwa hiyo, kila siku, mtu anapaswa kuchunguza maisha yake na kutambua mapungufu na udhaifu wake. Kisha afanye juhudi kubwa kurekebisha maisha yake na kutimiza haki anazodaiwa na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) na viumbe.<\/p>\n<p>Baada ya swala yake tano ya kila siku, anatakiwa kuomba dua kwa Allah Ta\u2019ala<br \/>\nAmjalie tawfeeq ya kusimamisha Dini katika maisha yake yote.<\/p>\n<p>Miongoni mwa dua za mchana ambazo Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) aliufundisha ummah kuzisoma ni hizi zifuatazo:<\/p>\n<p class=\"\" dir=\"RTL\" style=\"text-align: center; font-family: 'Traditional Arabic'; font-size: 16pt;\">\u0627\u064e\u0644\u0644\u0651\u0670\u0647\u064f\u0645\u0651\u064e \u0627\u062c\u0652\u0639\u064e\u0644\u0652 \u062e\u064e\u064a\u0652\u0631\u064e \u0639\u064f\u0645\u064f\u0631\u0650\u064a\u0652 \u0622\u062e\u0650\u0631\u064e\u0647\u064f \u0648\u064e\u062e\u064e\u064a\u0652\u0631\u064e \u0639\u064e\u0645\u064e\u0644\u0650\u064a\u0652 \u062e\u064e\u0648\u064e\u0627\u062a\u0650\u064a\u0652\u0645\u064e\u0647\u064f \u0648\u064e\u062e\u064e\u064a\u0652\u0631\u064e \u0623\u064e\u064a\u0651\u064e\u0627\u0645\u0650\u064a\u0652 \u064a\u064e\u0648\u0652\u0645\u064e \u0623\u064e\u0644\u0652\u0642\u064e\u0627\u0643\u064e \u0641\u0650\u064a\u0652\u0647\u0650<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><em>Ewe Mwenyezi Mungu! Ifanye sehemu iliyo bora zaidi ya maisha yangu kuwa sehemu ya mwisho maishani mwangu, matendo bora zaidi ya maisha yangu kuwa matendo ya mwisho kabla sijaondoka duniani, na siku bora zaidi ya maisha yangu iwe siku nitakayokutana nawe.\u201d<\/em><\/p>\n<p>Allah Ta\u2019ala Atujaalie tawfeeq ya kurekebisha maisha yetu na kufuata Sunnah kamili ya Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam), na Allah Ta\u2019ala aijaalie siku iliyo bora zaidi ya maisha yetu kuwa siku ambayo tutakutana Naye.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Dawood bin Dinaar (rahimahullah) alikuwa Imaam mkubwa katika fani ya Hadithi na mwalimu wa Muhadditheen mashuhuri, mfano wa Imaam Shu\u2019bah ( rahimahullah) na Imaam Wakee\u2019 (rahimahullah). Wakati wa uhai wake, tauni ilikuwepo eneo la Khuraasaan alipokuwa akiishi. Kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa wameugua wakati wa tauni na wengi walipoteza maisha. Dawood bin Dinaar (rahimahullah) &hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":4,"featured_media":2119,"comment_status":"closed","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[29],"tags":[],"class_list":["post-3578","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","","category-bustani-ya-mapenzi"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3578","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/4"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=3578"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3578\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3590,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3578\/revisions\/3590"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/2119"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=3578"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=3578"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=3578"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}