{"id":3569,"date":"2026-07-25T16:05:35","date_gmt":"2026-07-25T14:05:35","guid":{"rendered":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3569"},"modified":"2026-08-13T12:35:18","modified_gmt":"2026-08-13T10:35:18","slug":"sunna-na-adabu-kusafiri","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3569","title":{"rendered":"Sunna Na Adabu Kusafiri 1"},"content":{"rendered":"<p>1. Kabla ya kuanza safari (yaani kusafiri kwenda sehemu ambayo ni kilomita 78 au zaidi), mtu anatakiwa kuswali rakaa mbili. Swalaah hii inajulikana kama Swalaatus Safar.<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><em>Mut\u2019im bin Miqdaam (rahimahullah) anasimulia kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: \u201cHakuna kitendo ambacho mtu anaweza kukiacha pamoja na familia yake kabla ya kuanza safari ambayo ni kheri zaidi kuliko rakaa mbili (Swalatus Safar) watakayoiswali.\u201d<\/em><\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><em>Imepokewa kwamba wakati wowote Ibnu Umar (Radhiyallahu anhuma) alipokusudia kuanza safari, alikuwa anaenda msikitini kwanza na kuswali.<\/em><\/p>\n<p>2. Kutana na wanafamilia na marafiki zako kabla ya kuanza safari (kama unaposafiri kwa ajili ya umrah au hajj) na uwaombe wakuombee dua.<\/p>\n<p><em>Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (Radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: \u201cMmoja wenu anapotaka kusafiri basi anapaswa kukutana na ndugu zake Waislamu (yaani familia na marafiki na kuomba wamuombee dua). Hakika dua yao iliyoongezwa pamoja na dua yake itakuwa ni njia ya yeye kupata wema (wakati wa safari yake).<\/em><\/p>\n<p>3. Wajulishe familia yako sehemu unapokwenda na mahali unapoishi wakati wa safari yako ili iwe rahisi kwao kuwasiliana nawewe.<\/p>\n<p>4. Wakati wa kuondoka, soma dua ya masnoon ya safar:<\/p>\n<p class=\"\" dir=\"RTL\" style=\"text-align: center; font-family: 'Traditional Arabic'; font-size: 16pt;\">\u0628\u0650\u0633\u0652\u0645\u0650 \u0627\u0644\u0644\u0647\u0650 \u0627\u064e\u0644\u0652\u062d\u064e\u0645\u0652\u062f\u064f \u0644\u0650\u0644\u0651\u0670\u0647 \u0633\u064f\u0628\u0652\u062d\u064e\u0627\u0646\u064e \u0627\u0644\u0651\u064e\u0630\u0650\u064a\u0652 \u0633\u064e\u062e\u0651\u064e\u0631\u064e \u0644\u064e\u0646\u064e\u0627 \u0647\u0670\u0630\u064e\u0627 \u0648\u064e\u0645\u064e\u0627 \u0643\u064f\u0646\u0651\u064e\u0627 \u0644\u064e\u0647\u064f \u0645\u064f\u0642\u0652\u0631\u0650\u0646\u0650\u064a\u0652\u0646\u064e\u00a0 \u0648\u064e\u0625\u0650\u0646\u0651\u064e\u0627 \u0625\u0650\u0644\u0670\u0649 \u0631\u064e\u0628\u0651\u0650\u0646\u064e\u0627 \u0644\u064e\u0645\u064f\u0646\u0652\u0642\u064e\u0644\u0650\u0628\u064f\u0648\u0652\u0646\u064e \u0627\u064e\u0644\u0652\u062d\u064e\u0645\u0652\u062f\u064f \u0644\u0650\u0644\u0651\u0670\u0647 \u0627\u064e\u0644\u0652\u062d\u064e\u0645\u0652\u062f\u064f \u0644\u0650\u0644\u0651\u0670\u0647 \u0627\u064e\u0644\u0652\u062d\u064e\u0645\u0652\u062f\u064f \u0644\u0650\u0644\u0651\u0670\u0647 \u0627\u064e\u0644\u0644\u0647\u064f \u0623\u064e\u0643\u0652\u0628\u064e\u0631\u064f \u0627\u064e\u0644\u0644\u0647\u064f \u0623\u064e\u0643\u0652\u0628\u064e\u0631\u064f \u0627\u064e\u0644\u0644\u0647\u064f \u0623\u064e\u0643\u0652\u0628\u064e\u0631\u064f \u0644\u064e\u0627 \u0625\u0650\u0644\u0670\u0647\u064e \u0625\u0650\u0644\u0651\u064e\u0627 \u0627\u0644\u0644\u0647\u064f \u0633\u064f\u0628\u0652\u062d\u064e\u0627\u0646\u064e\u0643\u064e \u0627\u0644\u0644\u0651\u0670\u0647\u064f\u0645\u0651\u064e \u0625\u0650\u0646\u0651\u0650\u064a\u0652 \u0638\u064e\u0644\u064e\u0645\u0652\u062a\u064f \u0646\u064e\u0641\u0652\u0633\u0650\u064a\u0652 \u0641\u064e\u0627\u063a\u0652\u0641\u0650\u0631\u0652 \u0644\u0650\u064a\u0652 \u0641\u064e\u0625\u0650\u0646\u0651\u064e\u0647\u064f \u0644\u064e\u0627 \u064a\u064e\u063a\u0652\u0641\u0650\u0631\u064f \u0627\u0644\u0630\u0651\u064f\u0646\u064f\u0648\u0652\u0628\u064e \u0625\u0650\u0644\u0651\u064e\u0627 \u0623\u064e\u0646\u0652\u062a\u064e<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><em>Kwa jina la Allah Ta&#8217;ala. Sifa zote njema ni za Allah Ta\u2018ala, Ametakasika Allah Ta\u2019ala ambaye amemtiisha mnyama huyu (au akiweka gari hili chini ya udhibiti wetu) na hali sisi hatukuweza kulidhibiti (bila ya msaada Wake). Hakika sisi tutarejea kwa Mola wetu. Sifa njema zote ni za Allah Ta\u2018ala. Sifa njema zote ni za Allah Ta\u2019ala. Sifa njema zote ni za Allah Ta\u2018ala. Allah Ta\u2019ala ndiye mkubwa zaidi. Allah Ta\u2019ala ndiye mkubwa zaidi. Allah Ta\u2019ala ndiye mkubwa zaidi. Hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah Ta\u2019ala. (Ewe Mwenyezi Mungu subhaanahu wata&#8217;ala) Wewe ni mtakatifu zaidi. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu, basi nisamehe, kwani hakuna anayesamehe madhambi isipokuwa Wewe.<\/em><\/p>\n<p>5. Ni vyema kuanza safari siku ya Alhamisi. Kwa hivyo, ikiwa inawezekana kwako kusafiri siku ya Alhamisi, basi unapaswa kuanza safari yako siku ya Alhamisi. Kuanza safari siku nyingine yoyote pia inajuzu.<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><em>Ka\u2019b bin Maalik (radhiyallahu anhu) alisema, \u201cIlikuwa ni tabia ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) kwamba anapokusudia kuanza safari, kwa kawaida alikuwa akiondoka siku ya Alhamisi.<\/em><\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><em>Ka\u2019b bin Maalik (radhiyallahu anhu) alisema, \u201c Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) aliondoka siku ya Alhamisi kwa ajili ya vita vya tabuk, na alikuwa akipenda kuondoka siku ya Alhamisi.\u201d<\/em><\/p>\n<p>6. Hakikisha kuwa una mahitaji ya kutosha kwa ajili ya safari k.m. petroli, nguo, pesa za matumizi n.k.<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><em>Imepokewa kwamba Ibnu Umar (Radhiyallahu anhuma) alisema, \u201cNi sehemu ya heshima na utukufu wa mtu kwamba anachukua riziki za kutosha wakati wa safari yake.\u201d<\/em><\/p>\n<p>7. Ikiwa unawaacha wanaokutegemea k.m. mke na watoto n.k. basi kabla ya kuondoka, hakikisha kwamba mipango ya kutosha inafanywa ili mahitaji yao yatimizwe wakati wa kutokuwepo kwako.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>1. Kabla ya kuanza safari (yaani kusafiri kwenda sehemu ambayo ni kilomita 78 au zaidi), mtu anatakiwa kuswali rakaa mbili. Swalaah hii inajulikana kama Swalaatus Safar. Mut\u2019im bin Miqdaam (rahimahullah) anasimulia kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: \u201cHakuna kitendo ambacho mtu anaweza kukiacha pamoja na familia yake kabla ya kuanza safari ambayo ni kheri zaidi &hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":4,"featured_media":3558,"comment_status":"closed","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[43,14],"tags":[],"class_list":["post-3569","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","","category-kusafiri","category-sunna-na-adabu"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3569","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/4"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=3569"}],"version-history":[{"count":4,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3569\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3598,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3569\/revisions\/3598"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/3558"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=3569"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=3569"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=3569"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}