{"id":3542,"date":"2026-07-08T12:27:59","date_gmt":"2026-07-08T10:27:59","guid":{"rendered":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3542"},"modified":"2026-07-08T12:28:57","modified_gmt":"2026-07-08T10:28:57","slug":"machozi-ya-toba-maji-ya-kusafisha-moyo","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3542","title":{"rendered":"Machozi ya Toba &#8211; Maji ya Kusafisha Moyo"},"content":{"rendered":"<p>Shah Ruknuddeen (rahimahullah) alikuwa ni Mwanachuoni mkubwa na mchamungu aliyeishi Multan. Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) alimkubali sana miongoni mwa watu wake. Siku ya Jumu\u2019ah, msikitini ilikua ikijaa na watu wanaokuja kutoka sehemu mbali mbali ili kunufaika kutoka kwake.<\/p>\n<p>Siku moja, mfalme, Ghiyaathuddeen Tughluq, alimgeukia mshauri wake, Moulana Zaheeruddeen, na akamuuliza, \u201cNimeona kwamba karaamah (miujiza) ya Shah Ruknuddeen (rahimahullah) inajulikana sana miongoni mwa watu. Moulana Zaheeruddeen (rahimahullah) alijibu, \u201cNi karamah gani inaweza kuwa kubwa zaidi kuliko ukweli kwamba bila yeye kuwaalika watu, makundi ya watu wankusanyika kwake!\u201d<\/p>\n<p>Moulana Zaheerudden (rahimahullah) anataja:<\/p>\n<p>Kwa kuwa mfalme alikuwa ameniuliza swali hili, nilihisi ni lazima nimpe jibu linalofaa. Walakini, ndani kabisa ya moyo wangu, sikuwa na uhakika na uchamungu wa Shah Ruknuddeen. Nilihisi kwamba labda watu hawaji kwake kwa sababu ya uchamungu wake. Badala yake, inawezekana kwamba ana amal (zoezi) ambalo kupitia hilo watu wanavutiwa naye. Kwa wazo hili akilini, niliamua kwamba niende kwa Shah Ruknuddeen (rahimahullah) siku iliyofuata ili kumjaribu na kubaini kama alikuwa mchamungu wa kweli au la.<\/p>\n<p>Niliamua kwamba nikikutana naye, ningemuuliza kuhusu hekima nyuma ya sheria fulani za dini. Hasa, nilikusudia kumuuliza juu ya hekima ya kuosha mikono, kusugua mdomo na kuingiza maji kwenye pua mwanzo wa wudhu.<\/p>\n<p>Baada ya kupanga hivyo, nilikwenda kulala, na nikiwa usingizini, niliona katika ndoto kwamba nilimtembelea Shah Ruknudden (rahimahullah). Nilipokutana naye, alinipokea kama mgeni na kunipa chakula kitamu ambacho nilikula.<\/p>\n<p>Nilipoamka asubuhi iliyofuata, nilishangaa sana kuhusu ndoto niliyokuwa nimeona, na nilishangaa zaidi kugundua kwamba bado naweza kuonja chakula kitamu kinywani mwangu! Kwa kweli, ladha ya chakula ilibaki kinywani mwangu siku nzima!<\/p>\n<p>Licha ya kuiona ndoto hii, moyo wangu haukuathirika na ndoto hio ya Shah Ruknudden (rahimahullah) na maoni yangu hayakubadilika. Niliwaza mwenyewe, \u201cWatu huona ndoto kila wakati, na shetani ana uwezo wa kumfanya mtu aone ndoto kama hii. Kwa hivyo, sipaswi kuzingatia ndoto hii. Hivyo, niliamua kukutana naye, nikiwa na wasiwasi moyoni mwangu.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Shah Ruknuddeen (rahimahullah) alikuwa ni Mwanachuoni mkubwa na mchamungu aliyeishi Multan. Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) alimkubali sana miongoni mwa watu wake. Siku ya Jumu\u2019ah, msikitini ilikua ikijaa na watu wanaokuja kutoka sehemu mbali mbali ili kunufaika kutoka kwake. Siku moja, mfalme, Ghiyaathuddeen Tughluq, alimgeukia mshauri wake, Moulana Zaheeruddeen, na akamuuliza, \u201cNimeona kwamba karaamah (miujiza) ya &hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":4,"featured_media":2017,"comment_status":"closed","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[29],"tags":[],"class_list":["post-3542","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","","category-bustani-ya-mapenzi"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3542","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/4"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=3542"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3542\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3543,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3542\/revisions\/3543"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/2017"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=3542"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=3542"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=3542"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}