{"id":3490,"date":"2026-05-14T07:03:51","date_gmt":"2026-05-14T05:03:51","guid":{"rendered":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3490"},"modified":"2026-05-19T13:34:39","modified_gmt":"2026-05-19T11:34:39","slug":"mchamungu-wa-wakati-wake-bishr-haafi-rahimahullah","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3490","title":{"rendered":"Mchamungu wa Wakati Wake &#8211; Bishr Haafi (rahimahullah)"},"content":{"rendered":"<p>Bishr Haafi (rahimahullah) alikuwa mchamungu mashuhuri katika zama zake. Wakati mmoja, mtu fulani alimuuliza, \u201cUmeipataje nafasi hii ya juu ya uchamungu na uadilifu tunayoiona?\u201d Katika kujibu, Bishr (rahimahullah) alitaja yafuatayo:<\/p>\n<p>Chochote ambacho nimebarikiwa nacho ni kupitia neema ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala). Hali yangu ya awali ilikuwa kwamba sikuwa mtu wa kujitolea kwa deen.<\/p>\n<p>Siku moja, nilipokuwa nikitembea, niliona kipande cha karatasi chini. Pindi nilipoiokota, nikakuta jina la Allah Ta&#8217;ala limeandikwa juu yake. Niliinua macho yangu mbinguni na kusema, &#8220;Ewe Mwenyezi Mungu! Hili ni jina lako lililobarikiwa ambalo limetupwa chini!&#8221;<\/p>\n<p>Kisha nilisafisha karatasi na kuiweka mfukoni mwangu kwa heshima zote.<\/p>\n<p>Wakati huo, nilikuwa na dirham mbili tu. Nikaelekea kwenye duka la manukato, nikanunua manukato na kuipaka kwenye karatasi ile. Baada ya hapo, nilienda nyumbani, na kuiweka juu ya kabati.<\/p>\n<p>Usiku ule, niliota ndoto ambayo ndani yake niliambiwa, \u201cEwe Bishr! Umeinuwa jina letu basi sisi tutainuwa jina lako duniani na akhera.&#8221; Ilikuwa ni kwa ajili ya kitendo hiki ambapo Mwenyezi Mungu alinipa nafasi hii.<\/p>\n<p>Kutokana na tukio hili, tunaelewa kwamba wakati Bishr Haafi (rahimahullah) alionesha heshima kwenye jina la Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala), basi Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata\u2019alah) akambariki tawfeeq ya kubadilisha maisha yake.<\/p>\n<p>Mbali na hayo, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) Akambariki na ufahamu wa kweli wa Quran na Hadithi za Mtume (Sallallahu alaihi wasallam). Kwa hiyo, alihesabiwa miongoni mwa Muhaddithin wa zama zake.<\/p>\n<p>Huo ndio ulikuwa msimamo wake mkubwa hadi Imaam mkubwa wa zama zake Imam Ahmad bin Hanbal (rahimahullah) amesimulia Hadithi kutoka kwake na kufaidika na ujuzi wake wa kina.<\/p>\n<p>Maulamaa wanaeleza kuwa kuonyesha heshima kwa kitu chochote kile inayohusishwa na Dini (yaani Quran Majeed, Hadith, Msikiti, Adhaan, Maulamaa (masheikhe) , Huffaaz (wenye kuhifadhi Quran, n.k.) ni njia ya kupata baraka kubwa na kukubaliwa na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala).<\/p>\n<p><strong>Imam Ahmad bin Hanbal (rahimahullah) Akinufaika Kutoka Kwa Bishr Hafi (rahimahullah)<\/strong><\/p>\n<p>Tukio lifuatalo linatoa mwanga juu ya uelewa wa kina wa Dini na ma\u2019rifa (utambuzi) wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) ambayo Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) Amembariki nayo Bishr Hafi (rahimahullah), ambayo kwa ajili yake Imam Ahmad bin Hambal (rahimahullah) alimuiga:<\/p>\n<p>Wakati wa Imaam Ahmad bin Hambal (rahimahullah), kulikuwa na daktari fulani ambaye aliitwa Abdur Rahmaan At Tabeeb.<\/p>\n<p>Alikuwa akimtibu Imam Ahmad bin Hanbal na Bishr Hafi (Rahimahumallah) walipokuwa wagonjwa. Anasema:<\/p>\n<p>Wakati mmoja, Imam Ahmad bin Hanbal (rahimahullah) na Bishr Hafi (rahimahullah) walikuwa wagonjwa wote.<\/p>\n<p>Wakati wa kuwatibu wote wawili, niliona tofauti katika majibu wakati niliwauliza hali zao.<\/p>\n<p>Kila nilipomuuliza Bishr (rahimahullah) anajisikiaje, kwanza alikuwa akimtukuza Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) akisema \u201cAlhamdulillah\u201d, na kisha kunijulisha hali yake.<\/p>\n<p>Kinyume chake, kila nilipomuuliza Imam Ahmad bin Hanbal (rahimahullah), jinsi gani anavyojisikia, alikuwa akijibu tu kwamba alikuwa mzima. Hakunieleza ugumu halisi aliokuwa akipitia.<\/p>\n<p>Siku moja, nilimwambia Imaam Ahmad (rahimahullah) na kusema, \u201cNdugu yako, Bishr (rahimahullah), ni mgonjwa, na ninapomuuliza hali yake, huanza kwa kumhimidi Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) na kisha kunijulisha hali yake.<\/p>\n<p>\u201cLakini, ninapokuuliza kuhusu hali yako, unasema tu kwamba upo mzima.&#8221;<br \/>\nImaam Ahmad (rahimahullah) aliposikia haya, alisema, \u201cMuulize Bishr (rahimahullah) ni kwa nani amejifunza haya.\u201d<\/p>\n<p>Nilijibu, \u201cNinahisi vigumu kumuuliza swali kama hilo.\u201d Imaam Ahmad (rahimahullah) akaniambia, \u201cMwambie, \u2018Ndugu yako, Abu Abdillah (Imaam Ahmad) anataka kukuuliza ni kwa nani umejifunza haya.\u201d<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Bishr Haafi (rahimahullah) alikuwa mchamungu mashuhuri katika zama zake. Wakati mmoja, mtu fulani alimuuliza, \u201cUmeipataje nafasi hii ya juu ya uchamungu na uadilifu tunayoiona?\u201d Katika kujibu, Bishr (rahimahullah) alitaja yafuatayo: Chochote ambacho nimebarikiwa nacho ni kupitia neema ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala). Hali yangu ya awali ilikuwa kwamba sikuwa mtu wa kujitolea kwa deen. Siku &hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":4,"featured_media":2091,"comment_status":"closed","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[29],"tags":[],"class_list":["post-3490","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","","category-bustani-ya-mapenzi"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3490","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/4"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=3490"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3490\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3504,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3490\/revisions\/3504"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/2091"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=3490"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=3490"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=3490"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}