{"id":3462,"date":"2026-04-25T16:07:45","date_gmt":"2026-04-25T14:07:45","guid":{"rendered":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3462"},"modified":"2026-05-09T15:32:22","modified_gmt":"2026-05-09T13:32:22","slug":"nabi-isa-alaihis-salaam","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3462","title":{"rendered":"Nabi Isa (alaihis salaam)"},"content":{"rendered":"<p>Isa (\u2018alayhis salaam) ni Mtume wa Allah Ta\u2018ala na anahesabiwa miongoni mwa manabii wa daraja la juu. Allah Ta\u2019ala alimteremshia Injili (Biblia) na akamjalia na Shari\u2019ah. Yeye ndiye Nabii aliyetumwa duniani kabla ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam).<\/p>\n<p>Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: \u201cManabii wote ni kama ndugu wa baba mmoja, mama zao wanatofautiana, na Dini yao ni moja (yaani wote wanaamini tauheed \u2013 umoja wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala), ingawa Shari\u2019ah zao ni tofauti). Mimi ndiye mtu wa karibu sana wa Nabii Isa bin Maryam (\u2018alayhis salaam), kwa sababu hakuna Nabii baina yetu. Hakika Nabii Isa (\u2018alayhis salaam) atashuka.\u201d\u00a0(Musnad Ahmed #9270)<\/p>\n<p>Allah Ta\u2019ala alimtuma Nabii Isa (\u2018Alayhis Salaam) kwa Bani Israa\u2019il, lakini hawakumuamini na wakamkataa. Walijaribu hata kumuua, lakini Allah Ta\u2019ala akamlinda na akamnyanyua mbinguni akiwa hai. Hivi sasa, Nabii Isa (\u2018Alayhis Salaam) yupo hai mbinguni, na kabla ya Qiyaamah, Allah Ta\u2019ala atamrudisha duniani.<\/p>\n<p>Katika Hadith, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) amesema, \u201cNaapa kwa Yule ambaye maisha yangu yapo mkononi mwake! Nabii Isa (\u2018alayhis salaam)) atashuka kutoka mbinguni, na atatawala miongoni mwenu kama mtawala mwadilifu. Atauvunja msalaba na kuua nguruwe\u2026\u201d\u00a0(Sahih Muslim #155)<\/p>\n<p><strong>Kushuka kwa Nabii Isa (\u2018alaihis salaam) \u2013 Dalili Kubwa ya Qiyaamah<\/strong><\/p>\n<p>Kuteremka kwa Nabii Isa (\u2018alayhis salaam) kutoka mbinguni kuja duniani inahesabiwa miongoni mwa alama kuu za Qiyaamah.<\/p>\n<p>Katika Qur-aan Majeed, Allah Ta\u2018ala Anasema, \u201cNa hakika yeye (Nabii Isa [alayhis salaam]) ni chanzo cha kupata elimu ya Saa ya Mwisho (yaani kushuka kwake ni dalili ya Qiyaamah), basi usiwe na shaka juu yake (Saa ya Mwisho ya Qiyaamah kutokea)\u2026 (Sura Zukhruf aya 61)<\/p>\n<p>Katika Hadith moja, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) ametaja, \u201cHakika Qiyaamah hakitotokea mpaka muone kabla yake ishara kuu kumi. Moshi (aina ya ukungu au moshi utakaoshuka duniani kutoka mbinguni kabla ya Qiyaamah ambapo Waislamu watapata homa na makafiri watapoteza fahamu), kutokea kwa Dajjaal, mnyama kujitokeza, kuchomoza kwa jua kutoka magharibi, kushuka kwa Nabii Isa (\u2018alaihis salaam), Ya\u2019juuj na Ma\u2019juuj kutokea, sehemu tatu kuu duniani kuzama; kuzama mashariki, kuzama magharibi na kuzama katika Bara la Arabu. Alama ya mwisho ni moto utakaotokea Yemen na kuwapeleka watu kwenye uwanja wa kufufuliwa (Syria).\u00a0(Sahih Muslim #2901)<\/p>\n<p><strong>Imani ya Ahlus Sunnah wal Jamaa\u2019ah kuhusiana na Nabi Isa (\u2018alaihis salaam) kumuua Dajjaal.<\/strong><\/p>\n<p>Moja ya sababu kuu za Nabii Isa (\u2018alayhis salaam) kurudishwa duniani kabla ya Qiyaamah itakuwa ni kumuua Dajjaal. Nabii Isa (\u2018alaihis salaam) kumuua Dajjaal ni miongoni mwa imani za kimsingi za Ahlus Sunnah wal Jamaa\u2019ah.<\/p>\n<p>Allaamah Qadhi Iyaadh (rahimahullah) ametaja kuwa Nabii Isa (\u2018alaihis salaam) kurejea duniani kumuua Dajjaal ni miongoni mwa imani za kimsingi za Ahlus Sunnah wal Jamaa\u2019ah. Muhadditheen, Fuqahaa na Ulamaa wa Aqaa\u2019id wote wanakubali imani hii.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Isa (\u2018alayhis salaam) ni Mtume wa Allah Ta\u2018ala na anahesabiwa miongoni mwa manabii wa daraja la juu. Allah Ta\u2019ala alimteremshia Injili (Biblia) na akamjalia na Shari\u2019ah. Yeye ndiye Nabii aliyetumwa duniani kabla ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam). Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: \u201cManabii wote ni kama ndugu wa baba mmoja, mama zao wanatofautiana, na Dini &hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":4,"featured_media":2802,"comment_status":"closed","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[35],"tags":[],"class_list":["post-3462","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","","category-dalili-za-qiyaamah"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3462","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/4"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=3462"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3462\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3484,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3462\/revisions\/3484"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/2802"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=3462"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=3462"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=3462"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}