{"id":3451,"date":"2026-04-14T11:24:00","date_gmt":"2026-04-14T09:24:00","guid":{"rendered":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3451"},"modified":"2026-05-07T06:59:14","modified_gmt":"2026-05-07T04:59:14","slug":"mchamungu-mkubwa-fudhail-bin-iyaaz-rahimahullah","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3451","title":{"rendered":"Mchamungu Mkubwa &#8211; Fudhail bin Iyaaz (Rahimahullah)"},"content":{"rendered":"<p>Fudhail bin Iyaaz (Rahimahullah) alikuwa Muhaddith mashuhuri na mchamungu mkubwa wa zama zake.<\/p>\n<p>Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) alimbariki na daraja la juu katika Hadith kiasi kwamba Muhadditheen mashuhuri wengi, kama Abdullah bin Mubaarak, Sufyaan bin Uyainah na Imaam Shaafi\u2019i (Rahimahumullah) wamesimulia Hadith kutoka kwake.<\/p>\n<p>Imeripotiwa kwamba kabla ya Fudhail (rahimahullah) kubarikiwa na daraja la juu la uchamungu, alijulikana kuwa ni jambazi mashuhuri barabarani. Lakini, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) akajalia tawfiq ya kutubia dhambi zake na kurekebisha maisha yake.<\/p>\n<p><strong>Mfalme, Haarun Rasheed (rahimahullah), akifaidika na Ushauri wa Fudhail bin Iyaaz (Rahimahullah)<\/strong><\/p>\n<p>Imepokewa kwamba katika tukio moja, Haarun Rasheed (rahimahullah) alipohiji alimwambia Fadhl bin Rabi (rahimahullah), \u201cMimi naona udhaifu moyoni mwangu, basi nipeleke kwa mchamungu fulani ili nipate ushauri kutoka kwake na nifaidike kwake.\u201d<\/p>\n<p>Fadhl alipendekeza kwake kwamba waende kumuona Sufyaan bin Uyainah (rahimahullah). Walipofika nyumbani kwa Sufyaan (rahimahullah) na akagonga mlango wake, Sufyaan (rahimahullah) akampokea na heshima kubwa.<\/p>\n<p>Haarun Rashid (rahimahullah) akamwambia: \u201cMadhumuni ya kuja kwangu ni kutaka ushauri kutoka kwako.\u201d Sufyaan kisha akampa ushauri wa ujumla.<\/p>\n<p>Hatimaye, Haarun Rasheed (rahimahullah) alipotaka kuondoka, alimuuliza Sufyaan (rahimahullah), \u201cJe, una deni lolote ambalo ninaweza kukusaidia kulilipa?\u201d Sufyaan (rahimahullah) akajibu kwa kukubali, na Haarun Rasheed (rahimahullah) akamuagiza Fadhl amwambie alipe madeni yake.<\/p>\n<p>Baada ya kumuacha Sufyaan (rahimahullah), Haarun Rasheed (rahimahullah) alimgeukia Fadhl na kusema, \u201cSikunufaika na Sufyaan (rahimahullah) kwa namna nilivyotaka.\u201d (Huenda Haarun Rasheed (rahimahullah) hakutosheka kwa sababu alihisi kwamba Sufyaan (rahimahullah) alimuonesha heshima kubwa na hakumuonyesha udhaifu wowote) Hivyo basi Fadhl akapendekeza kwamba waende kumtembelea Imaam Abdur Razzaaq (rahimahullah).<\/p>\n<p>Imaam Abdur Razzaaq (rahimahullah) pia alimpokea Haarun Rashid (rahimahullah) kwa heshima kubwa na akampa nasaha za ujumla juu ya ombi lake.<\/p>\n<p>Kabla ya kuondoka, Haarun Rasheed (rahimahullah) akamuuliza, \u201cJe! una deni lolote ambalo ninaweza kukusaidia kulilipa?&#8221; Wakati Imaam Abdur Razzaaq (rahimahullah) alipojibu kwamba alikuwa na deni, Haaroon Rasheed alimuelekeza Fadhl alipe madeni hayo.<\/p>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<p>Kwa mara nyingine tena, walipoondoka, Haaroon Rasheed (rahimahullah) alimwambia Fadhl, \u201cSikunufaika na Imaam Abdur Razzaaq (rahimahullah) kwa namna nilivyotaka. Nitafutie mtu sahihi ambaye ninaweza kumrejelea.\u201d Kisha Fadhl akapendekeza kwamba waende kumtembelea Fudhail bin Iyaaz (Rahimahullah).<\/p>\n<p>Alipokutana na Fudhail (rahimahullah), Haarun Rasheed alimwomba ampe ushauri. Fudhail akamwambia, \u201cWakati Umar bin Abdil Aziz (rahimahullah) alipoteuliwa kuwa Khalifah, alimwita Saalim bin Abdillah, Muhammad bin Ka\u2019b na Rajaa bin Haywah (Rahimahumullah) akawaambia, \u2018Nimejaribiwa mtihani huu wa utawala, basi tafadhali nishaurini.\u2019\u201d<\/p>\n<p>Fudhail (rahimahullah) akasema, \u201cUmar bin Abdil Aziz alikuwa akiwa na wasiwasi sana na Khilaafah kiasi kwamba aliiona kuwa ni mtihani kwake, nanyie mnaiona kuwa ni baraka (na hamna fikra sawa na yeye).<\/p>\n<p>Fudhail (rahimahullah) akamuonya kwamba kama hatasimamia mambo ya Khilaafah kwa mujibu wa shari\u2019ah, basi atapata adhabu ya Jahannum. Hii onyo lilikuwa na athari kubwa kwa Haaruun Rasheed (rahimahullah) hadi akaanza kulia sana.<\/p>\n<p>Haarun Rasheed alipotaka kuondoka, alimuuliza Fudhail (rahimahullah), \u201cJe, una deni lolote ambalo ninaweza kukusaidia kulilipa?\u201d Fudhail akajibu, \u201cNdio, nina deni ambalo ni haki ninazo kwa Mola wangu. Ukitaka kunisaidia, basi unaweza kufanya hivyo.\u201d<\/p>\n<p>Haaroon Rasheed (rahimahullah) kisha akampa Fudhail akisema, \u201cHizi hapa dinari elfu moja. Zipokee kutoka kwangu kama zawadi na zitumie kwa wanaokutegemea.<\/p>\n<p>Fudhail (rahimahullah) akajibu, \u201cSubhaanallah! Nimekuonyesha njia ya kupata wokovu, na hivi ndivyo unavyonilipa? Wewe unatoa mali hii kwa mtu ambaye hana haja nayo. Unapaswa afadhali mpe yule anayehitaji.\u201d<\/p>\n<p>Wakati Haarun Rasheed na Fadhl (rahimahumullah) walipotoka nyumbani kwa Fudhail, Haarun Rasheed (rahimahullah) alimwambia Fadhl, \u201cEwe Fadhl, unapotaka kunipeleka kwa mchamungu basi nipeleke kwa mtu kama yeye! Yeye bila shaka ndiye kiongozi wa<br \/>\nWaislamu wote!\u201d<\/p>\n<p>Haarun Rasheed (rahimahullah) alifurahishwa sana na Fudhail (rahimahullah) kwa sababu ya sifa nzuri alizokuwa nazo \u2013 khofu yake ya kuwajibika huko Akhera, uchamungu wake wa hali ya juu, kutopendezwa kwake na dunia, kujitolea katika shari\u2019ah na Sunnah na ushauri wake wa dhati kwa mfalme kuhusu namna anavyopaswa kusimamia mambo ya Khilaafah.<\/p>\n<p>Kimsingi, Haarun Rasheed (rahimahullah) alitoa ushahidi kwamba Fudhail (rahimahullah) alikuwa mtu wa Sunnah.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Fudhail bin Iyaaz (Rahimahullah) alikuwa Muhaddith mashuhuri na mchamungu mkubwa wa zama zake. Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;ala) alimbariki na daraja la juu katika Hadith kiasi kwamba Muhadditheen mashuhuri wengi, kama Abdullah bin Mubaarak, Sufyaan bin Uyainah na Imaam Shaafi\u2019i (Rahimahumullah) wamesimulia Hadith kutoka kwake. Imeripotiwa kwamba kabla ya Fudhail (rahimahullah) kubarikiwa na daraja la juu &hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":4,"featured_media":2091,"comment_status":"closed","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[29],"tags":[],"class_list":["post-3451","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","","category-bustani-ya-mapenzi"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3451","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/4"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=3451"}],"version-history":[{"count":5,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3451\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3480,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3451\/revisions\/3480"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/2091"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=3451"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=3451"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=3451"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}