{"id":3442,"date":"2026-04-11T16:41:20","date_gmt":"2026-04-11T14:41:20","guid":{"rendered":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3442"},"modified":"2026-04-11T16:42:44","modified_gmt":"2026-04-11T14:42:44","slug":"kiwango-cha-uadilifu-na-kuridhika-ndani-ya-utawala-wa-mahdi-radhiya-allaahu-anhu","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3442","title":{"rendered":"Kiwango cha Uadilifu na Kuridhika ndani ya Utawala wa Mahdi (Radhiya Allaahu \u2018anhu)"},"content":{"rendered":"<p>Katika baadhi ya hadithi, imeandikwa kwamba Mahdi (Radhiya Allaahu \u2018anhu) atatawala kwa uadilifu kiasi kwamba wakaazi wa mbingu na ardhi watakuwa radhi naye, na popote atakapokwenda duniani, Allah Ta\u2018ala atasababisha wema na baraka kushinda. Uadilifu wake utawazunguka watu wote na atawatawala kwa mujibu wa Sunnah ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam).<\/p>\n<p>Kwa ajili ya uadilifu wake, atakapomuelekeza mtu kutangaza, \u201cMwenye haja aje kwangu,\u201d atakuja mtu mmoja tu (kama vile mahitaji ya watu wengine wote yatakuwa yametimizwa kutokana na utawala wake wa haki).<\/p>\n<p>Abu Sa\u2019eed Khudri (Radhiya Allaahu \u2018anhu) anasimulia kwamba siku moja, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) aliwahutubia Maswahabah (Radhiya Allaahu \u2018anhum) akisema, \u201cNakupa bashara njema ya Mahdi (Radhiyallahu \u2018anhu) akija kwenye ummah huu (kabla ya Qiyaamah)! Atatumwa kwa ummah huu katika wakati ambapo ikhtilafu baina ya ummah zitakuwa nyingi na matetemeko ya ardhi yatashuhudiwa duniani. Atatawala kwa namna ambayo dunia itajawa na uadilifu, kama vile hapo awali ilivyokuwa imejaa na uonevu na dhuluma. Wakaao mbinguni na wakaao duniani watakuwa radhi naye. Atagawanya mali kwa usahihi.&#8221;<\/p>\n<p>Kisha Swahaabi mmoja (Radhiya Allaahu \u2018anhu) akamuuliza Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), \u201cEwe Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam)! Nini maana ya Mahdi (Radhiya Allaahu \u2018anhu) atagawanya mali kwa usahihi?\u201d Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akajibu: \u201cIna maana kwamba atagawanya mali kwa usawa na uadilifu baina ya watu.\u201d<\/p>\n<p>Kisha Rasulullah (Sallallahu alihi wasalllam) akaendelea, \u201cWakati huo, Allah Ta\u2019ala atajaza nyoyo za umma wa Muhammad (Sallallahu alaihi wasallam) kuridhika na furaha. Utawala wa uadilifu wa Mahdi (Radhiya Allaahu \u2018anhu) utawazunguka watu, mpaka watu watapata baraka kubwa kupitia kwake, kiasi kwamba mtu atawahutubia watu akisema, \u2018Ni mtu yupi miongoni mwenu mwenye haja ya mali?\u2019 Kutoka kwa watu wote, ni mtu mmoja tu atakayesimama na kusema, \u2018Mimi niko na mahitaji ya mali!\u2019<\/p>\n<p>\u201cMtu huyo atamwambia, \u2018Nenda kwa mweka hazina na umwambie, \u2018Mahdi amekupa maagizo ya kunipa mali.\u2019 Atakapokuja kwa mweka hazina, mtunza hazina atamwambia, \u2018Chukua mali kwa mikono yako miwili, kadiri unavyotaka!\u2019 Mtu huyo atachukua mali na mikono yote miwili akizikusanya mbele yake.<\/p>\n<p>\u201cWakati huo, mtu huyo atajuta na kusema, \u2018Mimi nilikuwa mwenye kutamani sana mali zaidi katika umma wa Muhammad (Sallallahu alaihi wasallam)! Je, hayo yaliyowatosheleza hayawezi kunitosheleza?\u2019 Akisema hivi, anarudisha mali. Lakini, mali atakayotaka kuirejesha kwa Mahdi (Radhiyallahu \u2018anhu) haitakubaliwa kutoka kwake, na ataambiwa, \u2018Tunachotoa haturudishi.\u2019<\/p>\n<p>&#8220;Sharti hii ya baraka itaendelea kuwepo katika muda wote wa Mahdi ambao ni miaka saba, minane au tisa.&#8221; (Majma\u2019uz Zawaa\u2019id #12393)<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Katika baadhi ya hadithi, imeandikwa kwamba Mahdi (Radhiya Allaahu \u2018anhu) atatawala kwa uadilifu kiasi kwamba wakaazi wa mbingu na ardhi watakuwa radhi naye, na popote atakapokwenda duniani, Allah Ta\u2018ala atasababisha wema na baraka kushinda. Uadilifu wake utawazunguka watu wote na atawatawala kwa mujibu wa Sunnah ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam). Kwa ajili ya uadilifu wake, &hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":4,"featured_media":3259,"comment_status":"closed","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[35],"tags":[],"class_list":["post-3442","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","","category-dalili-za-qiyaamah"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3442","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/4"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=3442"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3442\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3443,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3442\/revisions\/3443"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/3259"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=3442"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=3442"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=3442"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}