{"id":3073,"date":"2025-07-14T11:29:32","date_gmt":"2025-07-14T09:29:32","guid":{"rendered":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3073"},"modified":"2025-07-15T11:40:55","modified_gmt":"2025-07-15T09:40:55","slug":"3073","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=3073","title":{"rendered":"Nafasi ya juu ya Sa&#8217;eed bin Zaid (Radhiyallahu &#8216;Anhu) kati ya watu wa Madinah Munawwarah"},"content":{"rendered":"<p><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" class=\"alignnone wp-image-3076 size-full\" src=\"https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2025\/07\/Swahili_115_6.jpg\" alt=\"\" width=\"1080\" height=\"1080\" srcset=\"https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2025\/07\/Swahili_115_6.jpg 1080w, https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2025\/07\/Swahili_115_6-300x300.jpg 300w, https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2025\/07\/Swahili_115_6-1024x1024.jpg 1024w, https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2025\/07\/Swahili_115_6-150x150.jpg 150w, https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2025\/07\/Swahili_115_6-768x768.jpg 768w, https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2025\/07\/Swahili_115_6-200x200.jpg 200w\" sizes=\"auto, (max-width: 1080px) 100vw, 1080px\" \/><\/p>\n<p>Katika kipindi cha khilaafah yake, Mu&#8217;aawiyah (Radhiyallahu &#8216;Anhu) aliandika barua kwa Marwaan bin Hakam &#8211; waziri wake aliemchagua juu ya Madinah Munawwarah &#8211; ambaye yeye alimwagiza achukue Bay&#8217;ah (ahadi ya utii) kutoka kwa watu wa Madinah Munawwarah kwa niaba ya mtoto wake, Yazeed bin Mu&#8217;aawiyah, ambaye alikuwa Khalifah baada yake. Mu&#8217;aawiyah (Radhiyallahu &#8216;Anhu) hakuwa na ufahamu wa vitendo vibaya vya mtoto wake Yazeed, na kwa hivyo alitaka kumchagua kama mrithi wake kwa Khilaafah.<\/p>\n<p>Lakini, Marwaan hakuyatekeleza maagizo haya mara moja. Mtu wa Syria ambaye alikuwa huko Madinah Munawwarah wakati huo alimuuliza Marwaan sababu ya kuchelewesha kutekeleza maagizo ya Mu&#8217;aawiyah (Radhiyallahu &#8216;Anhu). Marwaan alijibu akisema, &#8220;Namsubiri Sa&#8217;eed bin Zaid (Radhiyallahu &#8216;Anhu) ili aje na achukuwe bay&#8217;ah, kwani anachukuliwa kama kiongozi wa watu na mtu mashuhuri kati ya watu wa Madinah Munawwarah. Ikiwa atachukuwa bay&#8217;ah kwa Yazeed, basi watu wengine watamfuata.&#8221;<\/p>\n<p>Mtu wa Syria huyo kisha akasema, &#8220;Kwa nini siendi na kumleta kwako ili aweze kufanya bay&#8217;ah?&#8221; Alienda nyumbani kwa Saeed bin Zaid (Radhiyallahu &#8216;Anhu) na akamwagiza aje kwa Marwaan na afanye bay&#8217;ah kwa Yazeed.<\/p>\n<p>Sa&#8217;eed bin Zaid (Radhiyallahu &#8216;Anhu) akajibu, &#8220;Unaweza kurudi; nitakuja na kufanya bay&#8217;ah (ikiwa ninataka). &#8221;<\/p>\n<p>Mtu wa Syria alikasirika akisema, &#8220;Unapaswa kwenda sasa na kuchukuwa bay&#8217;ah, au sivyo nitakukata kichwa! &#8221;<\/p>\n<p>Sa&#8217;eed bin Zaid (Radhiyallahu &#8216;Anhu) akajibu, &#8220;Unaniita nichukuwe bay&#8217;ah kwa wale ambao tulipigana nao kwa sababu ya Uislamu.&#8221; Na maneno haya ulionyesha kwamba yeye alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza wa Rasulullah (Sallallahu &#8216;Alaihi Wasallam), kwa sababu hio alielewa kwamba mtu gani anayestahili kuchukuwa bay&#8217;ah kwake na mtu gani hafai, na bila shaka, Yazeed hakustahili kutimiza.<\/p>\n<p>Mtu huyo wa Syria kisha akarudi kwa Marwaan na kumweleza kile kilichotokea, ambacho Marwaan alimshauri abaki kimya na asiwafahamishe watu juu ya kile kilichopitishwa.<\/p>\n<p>Sa&#8217;eed (Radhiyallahu &#8216;Anhu) kwa hivyo alikataa kuja kuchukuwa bay&#8217;ah kwa Yazeed, na kwa hivyo Marwaan alimuacha nje na kuanza kuchukua bay&#8217;ah, kwa niaba ya Yazeed, kutoka kwa Watu wa Madinah Munawwarah.<\/p>\n<p>Baadaye, mke anayeheshimiwa wa Rasulullah (Sallallahu &#8216;Alaihi Wasallam), Ummu Salamah (Radhiyallahu&#8217; Anha) alifariki. Alikuwa ametoa wasiyya kwamba swala ya Janaazah yake ifanyike na Sa&#8217;eed bin Zaid (Radhiyallahu &#8216;Anhu). Kwa sababu ya upendeleo wake, Marwaan hakuenda mbele kuswalisha Swala ya janazah.<\/p>\n<p>Pindi alipomsubiria Sa&#8217;eed bin Zaid, mtu huyo wa Syria alimuuliza Marwaan, &#8220;Kwanini hukwenda mbele kuongoza Janaazah? &#8221; Marwaan akajibu, &#8220;Ninamgojea mtu ambaye ulikuwa umekusudia kumtoa kichwa (wakati hakutaka kuja mbele kuchukuwa bay&#8217;ah kwa Yazeed),&#8221; Marwaan alisema haya kwa kumzingatia Sa&#8217;eed bin Zaid (Radhiyallahu &#8216;Anhu).<\/p>\n<p>Kusikia hili, mtu huyo wa Syria aligundua nafasi ya juu wa Sa&#8217;eed na hapo hapo akafanya istighfaar, akiomba msamaha wa Allah Ta&#8217;ala kwa makosa aliyoyafanya kwa sa&#8217;eed. <em>(Tareekh Ibnu Asaakir 21\/88, Mustadrak #5853 na al-Mu&#8217;jamul Kabeer #345)<\/em><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Katika kipindi cha khilaafah yake, Mu&#8217;aawiyah (Radhiyallahu &#8216;Anhu) aliandika barua kwa Marwaan bin Hakam &#8211; waziri wake aliemchagua juu ya Madinah Munawwarah &#8211; ambaye yeye alimwagiza achukue Bay&#8217;ah (ahadi ya utii) kutoka kwa watu wa Madinah Munawwarah kwa niaba ya mtoto wake, Yazeed bin Mu&#8217;aawiyah, ambaye alikuwa Khalifah baada yake. Mu&#8217;aawiyah (Radhiyallahu &#8216;Anhu) hakuwa na &hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":4,"featured_media":3076,"comment_status":"closed","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[25],"tags":[],"class_list":["post-3073","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","","category-sahaabah"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3073","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/4"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=3073"}],"version-history":[{"count":5,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3073\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":3079,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/3073\/revisions\/3079"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/3076"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=3073"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=3073"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=3073"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}