{"id":2407,"date":"2024-05-21T07:42:12","date_gmt":"2024-05-21T05:42:12","guid":{"rendered":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=2407"},"modified":"2024-06-04T12:10:46","modified_gmt":"2024-06-04T10:10:46","slug":"swalaah-ufunguo-wa-jannah","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/sw.alislaam.com\/?p=2407","title":{"rendered":"Swalaah \u2013 Ufunguo wa Jannah"},"content":{"rendered":"<p>Uislamu ndio njia pekee inayoongoza kwenye mapenzi ya Allah Ta&#8217;ala na inaongoza kwenye Jannah. Kupitia Uislamu, mtu atapata radhi za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;aala) na kupata mafanikio ya milele.<\/p>\n<p>Katika faradhi zote za Uislamu, faradhi ya Swalaah ipo na daraja ya juu zaidi. Mtume (Sallallahu &#8216;alaihi wasallam) amesema: &#8220;Swalah ni ufunguo wa Jannah.&#8221;<\/p>\n<p>Katika Hadith nyingine, Mtume (Sallallahu &#8216;alaihi wasallam) amesema: \u201cSwala ni nuru.\u201d Kwa hivyo, ikiwa mtu anataka kumulika maisha yake, basi aangazie maisha yake na Swalaah.<\/p>\n<p>Hivi sasa, nchi nyingi kote ulimwenguni zinakabiliwa na shida na pia uchumi mdogo. Katika kukabiliana na msukosuko huu wa kimataifa, mipango na mifumo mbalimbali inapitishwa ili kukuza uchumi.<\/p>\n<p>Lakini, katika Quraan Takatifu na Hadith, Allah Ta&#8217;ala na Mtume Wake (sallallahu &#8216;alaihi wasallam) wameunganisha baraka za riziki na Swalaah.<\/p>\n<p>Ndani ya Qur-aan Takatifu, Allah Ta&#8217;ala Anasema:<\/p>\n<p class=\"\" dir=\"RTL\" style=\"text-align: center; font-family: usmaan_taha; font-size: 16pt; line-height: 38px;\">\u0648\u064e\u0623\u0652\u0645\u064f\u0631\u0652 \u0623\u064e\u0647\u0652\u0644\u064e\u0643\u064e \u0628\u0650\u0627\u0644\u0635\u0651\u064e\u0644\u064e\u0627\u0629\u0650 \u0648\u064e\u0627\u0635\u0652\u0637\u064e\u0628\u0650\u0631\u0652 \u0639\u064e\u0644\u064e\u064a\u0652\u0647\u064e\u0627<span class=\"sign\">\u00a0\u06d6<\/span>\u00a0\u0644\u064e\u0627 \u0646\u064e\u0633\u0652\u0623\u064e\u0644\u064f\u0643\u064e \u0631\u0650\u0632\u0652\u0642\u064b\u0627<span class=\"sign\">\u00a0\u06d6<\/span>\u00a0\u0646\u0651\u064e\u062d\u0652\u0646\u064f \u0646\u064e\u0631\u0652\u0632\u064f\u0642\u064f\u0643\u064e<span class=\"sign\">\u00a0\u06d7<\/span>\u00a0\u0648\u064e\u0627\u0644\u0652\u0639\u064e\u0627\u0642\u0650\u0628\u064e\u0629\u064f \u0644\u0650\u0644\u062a\u0651\u064e\u0642\u0652\u0648\u064e\u0649\u0670\u00a0<span class=\"ayaNumber\">\u200e\ufd3f\u0661\u0663\u0662\ufd3e\u200f<\/span><\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><em>Waamrishe familia yako kuswali na uwe na msimamo juu yake (wewe mwenyewe). Hatukuombi riziki wewe &#8211; sisi ndo tunakuruzuku.<\/em><\/p>\n<p>Abdullah bin Salaam (radhiyallahu &#8216;anhu) anasimulia kwamba wakati wowote nyumba ya Mtume (sallallahu &#8216;alaihi wasallam) ilipokuwa ikikumbwa na matatizo ya kifedha, Mtume (Sallallahu &#8216;alaihi wasallam) alikuwa akiwahimiza kukimbilia kwenye Swalah na pia kuwasomea aya iliyotajwa hapo juu.<\/p>\n<audio class=\"wp-audio-shortcode\" id=\"audio-2407-1\" preload=\"none\" style=\"width: 100%;\" controls=\"controls\"><source type=\"audio\/mpeg\" src=\"https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/AUD-20240521-WA0000.mp3?_=1\" \/><a href=\"https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/AUD-20240521-WA0000.mp3\">https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/AUD-20240521-WA0000.mp3<\/a><\/audio>\n<p><strong>Nguzo ya Kituo cha Dini<\/strong><\/p>\n<p>Wakati mtu akisilimu, basi miongoni mwa mambo ya kwanza Mtume (sallallahu &#8216;alaihi wasallam) angemfundisha ni Swalaah.<\/p>\n<p>Maisha yote ya Mtume (sallallahu &#8216;alaihi wasallam) yaliwekwa kwa ajili ya kusimamisha Swalah katika ummah. Alipokuja Quba na Madinah Munawwarah, kipaumbele chake cha kwanza kabisa kilikuwa ni kusimamisha msikiti na kuwaunganisha kwa ajili ya swalah.<\/p>\n<p>Mbali na hayo, Rasulullah (sallallahu &#8216;alaihi wasallam) aliamuru kwamba msikiti ujengwe katika kila eneo ili kuwaunganisha watu juu ya swalah.<\/p>\n<p>Mtume (Sallallahu &#8216;alaihi wasallam) amesema: &#8220;Swala ni nguzo ya katikati ya Dini.&#8221; Kwa maneno mengine, kwa kulinda nguzo hii ya katikati, Dini nzima ya mtu italindwa, na kwa kuharibu nguzo hii ya katikati, muundo mzima wa Dini yake utaanguka.<\/p>\n<p>Aaishah (radhiyallahu &#8216;anha) alielezea mwenendo wa Mtume (Sallallahu &#8216;alaihi wasallam) na umuhimu aliouonyesha wa kuswali msikitini. Anaripoti, &#8220;Ndani ya nyumba, Rasulullah daima alikuwa akisaidia kazi za nyumbani. Lakini mara tu aliposikia adhaan, alitoka nyumbani kwenda msikitini.\u201d<\/p>\n<p>Wakati mmoja, ujumbe wa Thaqief ulikuja kwa Rasulullah (sallallahu &#8216;alaihi wasallam) kwa nia ya kusilimu. Hata hivyo, waliomba rukhsa kutokwenda jihaad, kutokulipa ushr (kutoa asilimia kumi ya mazao) kwa mtoza zakaat na kutokuswali.<\/p>\n<p>Rasulullah (Sallallahu &#8216;alaihi wasallam) alikubali maombi yao mawili ya mwanzo, lakini akakataa kuwapa kibali cha kuacha kuswali. Mtume (Sallallahu &#8216;alaihi wasallam) amesema: \u201cHakuna kheri katika Dini ambayo haina Swalaah.<\/p>\n<audio class=\"wp-audio-shortcode\" id=\"audio-2407-2\" preload=\"none\" style=\"width: 100%;\" controls=\"controls\"><source type=\"audio\/mpeg\" src=\"https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/AUD-20240528-WA0000.mp3?_=2\" \/><a href=\"https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/AUD-20240528-WA0000.mp3\">https:\/\/sw.alislaam.com\/wp-content\/uploads\/2024\/05\/AUD-20240528-WA0000.mp3<\/a><\/audio>\n<p><strong>Umuhimu Wa Swalaah Ndani Ya Maisha Ya Umar (radhiyallahu &#8216;anhu)<\/strong><\/p>\n<p>Umuhimu wa Swalaah ulikuwa umeingia sana katika nyoyo za Maswahaba (radhiyallahu &#8216;anhum) kiasi kwamba hata walipokuwa kwenye kitanda chao cha kufa, walihakikisha kwamba wanaisimamisha nguzo ya Swalaah.<\/p>\n<p>Asubuhi ambayo Umar (radhiyallahu &#8216;anhu) alichomwa kisu, Miswar bin Makhramah (radhiyallahu &#8216;anhu) aliingia kwake. Alipoingia, alimkuta Umar (radhiyallahu &#8216;anhu) amepoteza fahamu.<\/p>\n<p>Miswar (radhiyallahu &#8216;anhu) akawauliza wale waliokuwepo Umar (radhiyallahu &#8216;anhu) alikuwa tayari ameswali. Walijibu kuwa bado hajapata fahamu, na kwa hivyo hajaswali.<\/p>\n<p>Miswar (radhiyallahu &#8216;anhu) alijua bidii ya Umar (radhiyallahu &#8216;anhu) katika Swalaah ndani ya maisha yake yote. Kwa hiyo, Miswar (radhiyallahu &#8216;anhu) akawausia kumwamsha kwa kumtajia kuwa ni wakati wa Swalaah. Kwa hiyo, wakasema: \u201cEwe Amirul-Mu\u2019minin, Swalaah yako!<\/p>\n<p>Mara tu Umar (radhiyallahu &#8216;anhu) aliposikia neno \u2018Swalaah\u2019, aliamka na kusema, \u201cNdiyo! Wallahi! Hakuna fungu katika Uislamu kwa yule anayepuuza Swalah yake!\u201d Umar (radhiyallahu &#8216;anhu) baada ya hapo akaswali.<\/p>\n<p>Umar (radhiyallahu &#8216;anhu) pia aliuliza, \u201cJe, watu waliswali Alfajiri?\u201d Aliambiwa kwamba watu waliswali. Hapo tu ndipo Umar (radhiyallahu &#8216;anhu) alihisi kutosheka.<\/p>\n<p>Allah (Subhaanahu wa Ta&#8217;ala) atujaalie tuwe na uwezo wa kuiga kila Sunnah ya Rasulullah (sallallahu &#8216;alaihi wasallam) katika kila nyanja ya maisha yetu.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Uislamu ndio njia pekee inayoongoza kwenye mapenzi ya Allah Ta&#8217;ala na inaongoza kwenye Jannah. Kupitia Uislamu, mtu atapata radhi za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata&#8217;aala) na kupata mafanikio ya milele. Katika faradhi zote za Uislamu, faradhi ya Swalaah ipo na daraja ya juu zaidi. Mtume (Sallallahu &#8216;alaihi wasallam) amesema: &#8220;Swalah ni ufunguo wa Jannah.&#8221; Katika Hadith &hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":4,"featured_media":2408,"comment_status":"closed","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[29],"tags":[],"class_list":["post-2407","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","","category-bustani-ya-mapenzi"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/2407","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/4"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=2407"}],"version-history":[{"count":6,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/2407\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":2461,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/2407\/revisions\/2461"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/2408"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=2407"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=2407"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/sw.alislaam.com\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=2407"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}